logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Viongozi wa Kenya Kwanza watilia shaka uchaguzi wa Agosti 9

''Tume ya uchaguzi na mipaka wanafaa kuhakikisha vifaa vya uchaguzi kufika maeneo tofauti kwa wakati unaofaa,''  Duale alisema

image
na Davis Ojiambo

Habari22 July 2022 - 13:00

Muhtasari


  • • Wanasiasa hao pia walidai kuwa hakuna usalama wa kutosha kwa maafisa wa Tume ya  uchanguzi na mipaka (IEBC).
  • • Wanataka Tume ya Uchaguzi na mipaka (IEBC) kuwahakikishia kwamba uchanguzi wa Agosti 9 utakuwa wa haki na huru.
Kinara wa ANC Musalia Mudavadi

Viongozi wa Kenya kwanza sasa wanataka Tume ya Uchaguzi na mipaka (IEBC) kuwahakikishia kwamba uchanguzi wa Agosti 9 utakuwa wa haki na huru.

Wakizungumza na wanahabari, viongozi hao walisema kuwa rais Uhuru Kenyatta ameenda kinyume na sheria za humu nchini kwa kujihushisha katika siasa.

''Nataka kumuuliza rais jinsi gani wewe na serikali yako ni mwaminifu kwa katiba ya Kenya, haswa kwa uchaguzi wetu wa kidemokrasia, uchaguzi huru na wa haki, je wewe ni mwaminifu kiasi gani'' Mudavadi aliuliza.

Wanasiasa hao pia walidai kuwa hakuna usalama wa kutosha kwa maafisa wa Tume ya  uchanguzi na mipaka (IEBC).

''Kuna mpango wa udanganyifu ya uchaguzi mkuu na wapinzani wetu, na tunafahamu ushirikiano walionao na wale wageni wa kigeni kuhusu uchaguzi, lakini hatutawaruhusu,'' Duale alisema.

Timu hiyo pia  iliwarai Wakenya kujitokeza na kupiga kura Agosti 9 bila wasiwasi wowote kwani wanaamini kuwa Naibu wa Rais William Ruto atashinda uchaguzi huo.

''Tutakuwa macho kuona jinsi uchaguzi utakavyoendeshwa ili kuepusha udanganyifu wa aina yoyote, Wakenya lazima wafahamiswe  kuhusu shughuli zote ya uchaguzi,'' Duale  alisema

Haya yalijiri baada ya Viongozi kutoka mirengo ya Kenya Kwanza kudai kuwa wanafahamu pia uwezokano wa Wapinzani wao kukuwa na kituo mbadala ya kujumuisha kura

''Tume ya uchaguzi na mipaka wanafaa kuhakikisha kuwa vifaa vya uchaguzi kufika maeneo tofauti kwa wakati unaofaa,''  Duale alisema

Pia walidai kuwa kukamatwa kwa raia wa Kigeni na baadhi vya stika ya IEBC ni mojawapo ya njia ambayo serikali inataka kutumia kuhakikisha kuwa uchaguzi isikuwe wa haki na huru

''Kama walikuwa na hatia ya kupatikana na hizo stakabadhi basi kisheria hawangewachwa,wangefikishwa mpaka mahakamani,lakini waliachiliwa badaye'' Wetangula alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved