Washukiwa watano wa genge mjini Kisumu wakamatwa na Polisi

Walidaiwa kunaswa kwenye CCTV wakiiba mali ya thamani ya Sh500,000 kutoka kwa duka la vifaa vya elektroniki

Muhtasari

•Dennis Odhiambo almaarufu Deno, Hillary Odero almaarufu Konza, Eugene Akello almaarufu Yujo, Alex Amena almaarufu Spanner Boy na Hassan Hussein almaarufu Marwa.

•Polisi wanasema ni wanachama wa kundi la magenge tisa ambalo limekuwa likiwahangaisha wakaazi wa Kisumu.
 

Baadhi ya washukiwa wa genge walikamatwa mjini Kisumu baada ya kudaiwa kuvamia duka la kielektroniki na kuiba bidhaa za thamani ya Sh500,000.
Baadhi ya washukiwa wa genge walikamatwa mjini Kisumu baada ya kudaiwa kuvamia duka la kielektroniki na kuiba bidhaa za thamani ya Sh500,000.
Image: STAR

Polisi wamewakamata vijana watano waliosema ni wanachama wa genge la wahalifu mjini Kisumu.

Ni Dennis Odhiambo almaarufu Deno, Hillary Odero almaarufu Konza, Eugene Akello almaarufu Yujo, Alex Amena almaarufu spanner boy na Hassan Hussein almaarufu Marwa.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Kisumu ya Kati Anthony Maina alisema washukiwa hao walivamia duka la vifaa vya elektroniki huko Riat katika kaunti ndogo ya Kisumu Magharibi mnamo Julai 6.

Washukiwa hao walionaswa na kamera ya CCTV waliiba mali ya thamani ya Sh500,000.

Kesi hiyo iliripotiwa katika kituo cha polisi cha Kogony mnamo Julai 8. Duka hilo ni la afisa wa gereza.

Maina alisema walikamatwa Jumatano na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Kondele wakiongozwa na OCS Fredrick Kirui.

Watu hao walikamatwa katika mzunguko wa Kondele, Koyango, Molem, Kayengo na Manyatta Arab

Wanashukiwa kuwa wanachama wa kundi la magenge tisa ambalo limekuwa likiwahangaisha wakazi wa Kisumu.

Mkuu huyo wa polisi alisema walikuwa wakiwafuata washukiwa wengine ambao bado hawajashikwa.

Polisi walikamata pikipiki moja ambayo washukiwa wanaodaiwa kutumia wakati wa msako huo.

Washukiwa wengi hutumia pikipiki kutekeleza shughuli zao za uhalifu. Watano hao watahamishiwa katika Kituo cha Polisi cha Maseno, kaunti ndogo ya Kisumu Magharibi kushtakiwa.