SRC yaondoa marupu rupu ya wabunge kuhudhuria vikao vya bunge

Muhtasari

• Tume ya kudhibiti mishahara nchini Kenya, SRC imetangaza kuondoa marupurupu yanayolipwa wabunge kila wanapohudhuria vikao vya bunge.

Mwenyekiti wa SRC Lyn Mengich Picha: MAKTABA
Mwenyekiti wa SRC Lyn Mengich Picha: MAKTABA

Tume ya kudhibiti mishahara nchini Kenya, SRC imetangaza kuondoa marupurupu yanayolipwa wabunge kila wanapohudhuria vikao vya bunge.

Mwenyekiti Lyn Mengich alitangaza hatua hiyo wakati wa mkutano na Chama cha Wahariri mjini Nairobi siku ya Alhamisi.

Mbali na mshahara wabunge na maseneta nchini Kenya hulipwa marupurupu ya shilingi 5000 kwa kila kikao cha bunge wanachohudhuria. 

Mengich alisema kwamba marufuku hiyo inaanza kutekelezwa kuanzia Agosti 9. 

Kulingana na SRC marufuku hii pia itaathiri Maspika na mawaziri katika serikali za kaunti. 

Mengich alibainisha kuwa marupurupu yaliyositishwa ni pamoja na yale ya usafiri kwa maeneo bunge na ruzuku ya magari kwa Maafisa wote wa Serikali.