Mfanyikazi apondwa na tenki ya mafuta hadi kufa Nairobi

Kwingineko, fundi mmoja aliuawa na nguvu za umeme katika eneo la Kasarani.

Muhtasari

•Mwathiriwa alikuwa miongoni mwa wafanyakazi waliokuwa wakishusha tanki katika Energy Petrol Station.

•Kwingineko, fundi mmoja aliuawa na nguvu za umeme katika eneo la Kasarani.

Crime Scene
Image: HISANI

Mfanyikazi mmoja aliuawa wakati tanki la mafuta la chuma alilokuwa akishusha kutoka kwa lori lilipomwangukia katika eneo la Shauri Moyo, Nairobi. 

Mwathiriwa alikuwa miongoni mwa wafanyakazi waliokuwa wakishusha tanki katika Energy Petrol Station kando ya Barabara ya General Waruinge wakati kisa hicho kilitokea Jumatatu alasiri. 

Marehemu alitambuliwa kwa jina la Harrison Nduku, 28, na polisi wanasema wanachunguza tukio hilo.  

Mkuu wa polisi wa Nairobi James Mugera alisema walipigiwa simu na kufahamishwa kuhusu tukio hilo punde baada ya kutokea. 

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti huku uchunguzi ukiendelea. 

Kwingineko, fundi mmoja aliuawa na nguvu za umeme katika eneo la Kasarani, Nairobi. 

Mfanyikazi mwingine alipata majeraha mabaya wakati ngazi waliyokuwa wakitumia ilipogusana na nyaya za moto. 

Wawili hao walikuwa wakitengeneza mifereji ya maji katika nyumba ya kibinafsi wakati kisa hicho kilipotokea. 

Mwili wa marehemu ulihamishiwa hadi chumba cha kuhifadhia maiti huku aliyejeruhiwa akikimbizwa hospitalini akiwa katika hali mbaya. 

Matukio kama haya yamekuwa yakiongezeka jijini huku ukosefu wa zana za usalama ukilaumiwa kwa mtindo huo.  

Viongozi wamekuwa wakitoa wito kwa watengenezaji kuhakikisha usalama wa wafanyikazi. Hii inafuatia kuongezeka kwa hali ya ajali mbaya katika tovuti kama hizo. 

Polisi wanasema wanarekodi ajali mbaya katika maeneo ya ujenzi kila siku na wanataka taasisi mbalimbali zilizopewa jukumu la kuhakikisha usalama wa wafanyikazi kuchukua hatua.