Afisa wa polisi mdogo alikamatwa baada ya kuripoti kwamba alipoteza bastola yake alipokuwa akiendesha pikipiki jijini Nairobi.
Polisi sasa wanatafuta bastola hiyo ambayo ilipotea katika Industrial Area Jumatatu usiku.
Afisa huyo alikamatwa baada ya kwenda kuripoti bastola yake iliyokuwa na risasi 14 ilitoweka baada ya kudondoka kutokwa kwa mfuko alipokuwa akiendesha pikipiki.
Polisi wanasema wanachunguza tukio hilo kwa lengo la kuchukua hatua zaidi kwa afisa huku msako ukiendelea.
Silaha kama hizo kawaida huishia kwenye mikono isiyofaa na kusababisha uharibifu.
Kwa mfano, bastola ambayo iliibiwa miaka minne iliyopita kutoka kwa afisa wa polisi baada ya kuwekewa dawa za kupoteza fahamu Nairobi ilihusishwa na visa 28 vya wizi jijini.
Washambuliaji waliokuwa wamechukua umiliki wa bastola hiyo aina ya Jericho baada ya kuibiwa kutoka kwa polisi mnamo Juni 20, 2019,katika eneo la Parklands, Nairobi, walilenga maduka ya Mpesa.
Silaha hiyo ilipatikana kutoka kwa washukiwa waliouawa mwezi Juni kando ya Northern Bypass.
Uchunguzi wa Bastola hiyo ulionyesha kuwa ilitumika katika visa 28 vya uhalifu 28 katika maeneo ya Kasarani, Makadara, Kayole, Kamukunji, Dandora, Buruburu, Ruai, Kikuyu, Embakasi na Karatina.
Silaha hiyo ilipatikana kutoka kwa wanaume watatu waliokuwa wameuawa na umati wa watu mnamo Juni 25, 2022, baada ya kumwibia mhudumu wa Mpesa huko Marurui, kando ya barabara ya Northern bypass.
Bunduki hiyo iliibiwa kutoka kwa afisa wa polisi ambaye alifanya kazi maalum katika kituo cha polisi cha Riruta. Hapo awali, alifanya kazi katika kituo cha polisi cha Parklands.
Alikuwa amewekewa mchele na kuachwa kwenye mtaro kabla ya silaha yake kuchukuliwa na washambuliaji.
Timu ya wapelelezi waliokuwa wakichambua kesi zilizotekelezwa na bastola hiyo walisema waligundua kuwa bunduki hiyo ilikuwa imekodishwa kwa majambazi kutoka Kayole, ambao kwa muda wa miaka minne iliyopita wamekuwa wakivamia maajenti wa Mpesa jijini.
Genge hilo lilishambulia na kuondoka kwa kasi kwa kutumia pikipiki.
Wengine wamepoteza maisha huku wengine wakiwa na alama za risasi za kudumu ambazo zitakuwa ukumbusho wa kusikitisha wa kukutana kwao na genge la umwagaji damu.
Maafisa wa polisi pia hawajasalimika huku wengine wakiendelea kuuguza majeraha, yaliyosababishwa na majambazi hao waliotoroka nyavu kadhaa za polisi.
Kwa kutumia bunduki hiyo, genge hilo liliiba takriban Sh10 milioni kutoka kwa maanjeti wa Mpesa pekee, DCI inasema.
Utafsiri: Samuel Maina