Msaidizi wa nyumba akamatwa kwa kunajisi watoto wa waajiri wake.

Maombi yake ya kuachwa huru hayakusikilizwa nakupelekwa katika Gereza la Wanawake la Langatta

Muhtasari

•Watoto wanajulikana kutotunza siri, kwa hivyo huyo mtoto wa miaka 5 aliambia huyo msaidizi mpya kuhusu tukio hilo  na mamake akasikia.

Sabina Mwikali Muasya kwenye mahakama
Sabina Mwikali Muasya kwenye mahakama
Image: HANDOUT

Mshukiwa wa kike mwenye umri wa miaka 22 kwa jina Sabina Mwikali Muasya alikamatwa na kufikishwa mahakamani na polisi baada ya kupatikana na hatia ya kunajisi watoto wa waajiri wake.

Kulingana na ushahidi, alitenda uhalifu huo alipokuwa akifanya kazi kwa bosi wake  mtaa wa Kileleshwa.

Ilisemekana alifanya kitendo hicho kwa kuwaingiza watoto katika chumba chake ya watumishi wa nyumbani wakati haukuwa na mtu mwingine kwenye boma hilo.

Pia ilidhihirishwa wazi kuwa  aliwahusisha watoto wadogo ambao walikuwa mvulana na msichana katika tendo la ndoa.

Mvulana huyo alikuwa na umri wa miaka 12 na msichana alikuwa na umri wa miaka 5 kulingana na ripoti  za kuaminika.

Ilisemekana kwamba Mwikali alimlazimisha mtoto huyo wa miaka 12 kujihusisha katika tendo la ndoa na dadake mwenye umri wa miaka 5.

Baadaye Mwikali aliondoka kwa nyuma hiyo baada ya kupata ujauzito na matendo yake hayakujulikana baadaye  wakati ambapo mfanyakazi mpya alipoajiriwa .

Mama ya watoto hao alijulia  kitendo hicho kiovu wakati akipita aliposikia mtoto  wake  wa miaka 5 akiwa na mazungumzo  na yule msaidizi mpya wa nyumba.

Watoto wanajulikana kutotunza siri, kwa hivyo huyo mtoto wa miaka 5 aliambia huyo msaidizi mpya kuhusu tukio hilo  na mamake akasikia.

Mama huyo alijawa na wasiwasi na kulazimika kupeleka mtoto wake hospitalini kwa uchunguzi wa kimatibabu.

Baadaye alitoa taarifa kwa polisi na operesheni ilifanywa na polisi na wakafanikiwa  kumkamata mshukiwa.

Baadaye mshukiwa alifikishwa mahakamani ambapo alikanusha mashtaka yote matatu aliyokuwa ameshtakiwa nayo yakiwemo ya ubakaji.

Aliiomba mahakama kuwa yeye ni mama anayenyonyesha mtoto wa miezi mitatu na hatakiwi kufungwa jela.

Maombi yake hayakusikilizwa alipopelekwa katika Gereza la Wanawake la Langatta hadi uamuzi utakapotolewa.