Msichana wa miaka 13 afariki kwa kujitoa uhai huko Kibera

Visa vya watu kujiua vimeongezeka mwaka huu

Muhtasari

•Mwanafunzi wa darasa la sita anasemekana alitumia shuka kujitoa uhai siku ya Jumanne.

Kitanzi
Kitanzi
Image: HISANI

Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha msichana mwenye umri wa miaka 13 ambaye anaripotiwa kufariki kwa kujitoa mhanga katika nyumba ya familia yao iliyoko Kibera, Nairobi.

Mwanafunzi wa darasa la sita anasemekana alitumia shuka kujitoa uhai siku ya Jumanne.

Kulingana na polisi, mtoto huyo alifunga shuka kwenye paa ili kujinyonga.

Mwili wake ulipatikana ukining’inia kutoka kwa paa mamake alipoenda kumwamsha baada ya kungundua kuwa amelala kwa muda.

Kesi mbili sawia za kujitoa mhanga huko Pangani na Buruburu pia ziliripotiwa kwa polisi Jumanne. Wahasiriwa ni pamoja na mwanamke aliyekufa alijinyonga.

Visa vya watu kujiua vimeongezeka mwaka huu na viongozi wanalaumu hali hiyo kuwa ni msongo wa mawazo.

 

Kwani maeneo mbali mbali vimeripotiwa kuadhirika sana kwa idadi ya vifo zikiwemo, Eregi, Kakamega, ambapo mwanume anayejulikana kama James Lirubi, 55, alifariki kwa kujinyonga nyumbani kwake huku katika eneo la Matungu, Vivian Warire mwenye umri wa miaka 21 akifariki kwa kujitoa uhai nyumbani kwake. Alikuwa mjamzito.

Kwingineko kulingana na polisi, mwanafunzi wa udaktari alifariki kwa kujinyonga katika chumba chake eneo la Nzambani, Seku, Kaunti ya Kitui. Mwili wa Brian Kipkoech ulipatikana katika chumba chake muda mrefu baada ya tukio hilo kutokea.

Na katika eneo la Sultan Hamud, Kaunti ya Makueni, mwili wa Philip Mutuku, 39, ulipatikana ukining’inia juu ya mti.

Chini ya Kifungu cha 226 cha Kanuni ya Adhabu, kujaribu kujiua ni kosa linaloadhibiwa kwa kifungo cha miaka miwili, faini au vyote kwa pamoja.