DCI wamtaka Moses Kuria kuandika taarifa kuhusu madai ya wizi wa kura

Walisema anafaa kufika katika afisi yoyote ya DCI iliyo karibu naye ili kuandika taarifa zaidi kuhusu anayoyajua.

Muhtasari
  • Hii ni baada ya madai aliyoandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusu njama ya kuiba kura

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria ameatakiwa kufika mbele ya afisi za DCI haraka iwezekanavyo.

Hii ni baada ya madai aliyoandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusu njama ya kuiba kura.

"DCI wamepata habari kuhusu chapisho la kuzua joto ambazlo linahusishwa na Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kurua akizungumzia madai mazito kuhusu kosa linalohusu uchaguzi," DCI ilisema.

Walisema anafaa kufika katika afisi yoyote ya DCI iliyo karibu naye ili kuandika taarifa zaidi kuhusu anayoyajua.

"DCI inamtaka mbunge huyo kuripoti kwa haraka katika kituo cha polisi au afisi za DCI zilizo karibu naye ili kuwezesha uchunguzi kufanywa na hatua kuchukuliwa. Taarifa kamili itasaidia pakubwa katika kuhakikisha kuwa hatua imechukuliwa," taarifa ya DCI iliongeza.