Huku baada ya DP Ruto kutangazwwa kuwa rais mteule na tume ya uchaguzi na mipaka siku ya Jumatatu, kupitia kwenye mitandao ya kijamii watu walitoa wito wa amani.
Mwimbaji wa Tanzania, Diamond Platnumz, Jumatatu alituma ujumbe wa pongezi kwa Wakenya kwa kukamilisha kwa amani zoezi la uchaguzi.
Platinumz alitumia ukurasa wake wa Instagram kuwaomba Wakenya kudumisha amani baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kumtangaza William Ruto kuwa rais mteule.
Mwanamuziki huyo aliwataka Wakenya kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuungana kwa manufaa ya taifa.
Sasa hivi si Team Ruto, Wajakoya ama Team Odinga, ni Pamoja Team Kenya,Ili kwa pamoja maendeleo ya Kenya na Wana Kenya Kwa Ujumla,” Aliandika Diamond.
Ujumbe wake Diamond unajiri baada ya viongozi wa kidini NCCK kuwaomba wakenya wadumishe amani wakati huu.