Gari la gavana Mutula lahusika kwenye ajali mnamo siku ya kuapishwa

Gari hilo lilipoteza udhibiti kabla ya kutua kwenye mtaro.

Muhtasari

•Ajali hiyo ilitokea katika Barabara ya Machakos-Wote karibu na Wote Town mwendo wa saa nne unusu asubuhi.

•Kilonzo alitumia gari tofauti kufika eneo la tukio la kuapishwa.

Gari la gavana mteule wa Makueni Mutula Kilonzo Junior lilihusika katika ajali likielekea kwenye hafla ya kuapishwa.
Gari la gavana mteule wa Makueni Mutula Kilonzo Junior lilihusika katika ajali likielekea kwenye hafla ya kuapishwa.
Image: MA3ROUTE

Gari la gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Junior lilihusika katika ajali kabla ya hafla ya kuapishwa kwake.

Ajali hiyo ilitokea katika Barabara ya Machakos-Wote karibu na Wote Town mwendo wa saa nne unusu asubuhi.

Duru za kuaminika ziliarifu kuwa watu watatu waliokuwa ndani waliweza kunusurika bila majeraha.

Mutula hakuwa miongoni mwa watu waliokuwa kwenye gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser V8 wakati ajali ilipotokea.

Gari la gavana mteule wa Makueni Mutula Kilonzo Junior lilihusika katika ajali likielekea kwenye hafla ya kuapishwa.
Gari la gavana mteule wa Makueni Mutula Kilonzo Junior lilihusika katika ajali likielekea kwenye hafla ya kuapishwa.
Image: MA3ROUTE

Kilonzo alitumia gari tofauti kufika eneo la tukio la kuapishwa.

Inasemekana gari hilo lilipoteza udhibiti kabla ya kutua kwenye mtaro.

Mengine yanafuata...