logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Arati ashtuka kugundua kaunti imeajiri madereva 256 ilhali magari ni 82 pekee

Arati  alisema atafanya uchunguzi kujua kila mmoja alivyopata kazi katika Kaunti hiyo.

image
na

Burudani01 September 2022 - 04:59

Muhtasari


•Baadhi ya walioajiriwa hawakuwa wamepewa majukumu katika kaunti hiyo, gavana Arati alisema.

•Gavana huyo alimwagiza afisa wa fedha wa Kaunti hiyo na wasimamizi wa magari kueleza utata huo bila mafanikio.

Gavana wa Kisii Simba Arati wakati wa kikao na wanahabari katika afisi ya eneo la Azimio mjini Kisumu Jumamosi.

Mnamo Jumatano, gavana wa Kisii Simba Arati alielezea kushtushwa na wafanyikazi walioajiriwa kama madereva katika kitengo cha ugatuzi.

Madereva 256 walikuwa wameajiriwa dhidi ya magari 82 yanayofanya kazi, alisema Arati.

Baadhi ya walioajiriwa hawakuwa wamepewa majukumu katika kaunti hiyo, gavana Arati alisema.

 Alisema atafanya uchunguzi kujua kila mmoja alivyopata kazi katika Kaunti hiyo.

Mkuu huyo wa Kaunti alikuwa akizungumza wakati wa mkutano na madereva katika Chuo cha Mafunzo ya Kilimo kilicho Kisii ya kati Jumatano alasiri.

Pia alifanya mkutano wa faragha na maafisa wakuu na watendaji wa kamati katika Farmers Resource Centre.

Alisema uongozi wake utahakikisha watumishi wote ambao wamekuwa wakitorosha umma fedha zake watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

"Ili kaunti iwe salama lazima maumivu yawe. Ni lazima tupiganie utimamu kwa gharama yoyote, hakutakuwa na njia za mkato," alisema.

Uchunguzi wa kawaida unaonyesha kuwa Kaunti imekuwa ikipoteza zaidi ya Sh6 milioni kwa wafanyikazi ambao hawajapatiwa majukumu.

“Hiki ni kiasi cha fedha ambacho upotevu ukizuiliwa kinaweza kutumika kujenga na kuandaa zahanati katika kijijini,” alikasirika.

 Katika kikao hicho, gavana huyo aliwataka afisa wa fedha wa Kaunti hiyo na wasimamizi wa magari kueleza utata huo bila mafanikio.

Gavana huyo alisema yuko tayari kuwachukulia hatua maafisa watakaobainika kukiuka sheria za uajiri na hivyo kuruhusu uvujaji wa pesa za umma isivyostahili.

"Haya ni maswala ambayo yanaomba majibu na lazima yashughulikiwe kwa watu huko mitaani ambao wanataka uongozi safi na wazi," Arati alisema.

Magari mengi hayakuwa yamesajiliwa kwa bima ya kina licha ya rekodi kutoka kwa idara ya fedha kuonyesha hivyo. Arati alisema ataangazia suala hilo siku chache zijazo ili kubaini kiwango cha upotevu wa kifedha kaunti hiyo.

Kwa hivyo aliamuru madereva wote na magari yao kukutana katika Uwanja wa Gusii siku ya Alhamisi kwa ajili ya kuhesabiwa kama sehemu ya kuanza kwa uchunguzi wa kina kuhusu kashfa za uajiri usio wa kawaida.

Arati zaidi aliwahimiza wafanyikazi kuripoti kwake dhuluma zozote wanazopitia wakati wa kazi yao.

"Nitafungua ofisi yangu ili mfanyakazi yeyote aingie kunishirikisha kicheshi kimoja au viwili. Ninaahidi kuwa sitawaangusha mkinipa taarifa za kijasusi zinazoweza kusaidia Kaunti hii kusonga mbele," aliongeza.

 Arati alisema ufisadi ungekuwa jambo la zamani anapoelekea kutia nidhamu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved