Jamaa asema kazi yake duniani imekamilika baada ya kumkatakata mamake hadi kufa

Mshukiwa alisemekana kuwa na matatizo ya kiakili kutokana na matumizi mabaya ya bangi kwa miaka mingi.

Muhtasari

•Mwanaume huyo anadaiwa kumkatakata mamake mwenye umri wa miaka 80 hadi kufa alijisalimisha kwa polisi na kutangaza kuwa amekamilisha kazi yake duniani.

•OCPD Mwangi alisema mkongwe huyo alitolewa nje ya nyumba yake, kisha kushambuliwa kwa panga.

Crime scene
Crime scene

Mwanamume mmoja kutoka Kinangop ambaye anadaiwa kumkatakata mamake mwenye umri wa miaka 80 hadi kufa alijisalimisha kwa polisi na kutangaza kuwa amekamilisha kazi yake duniani.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 41 alisemekana kuwa na matatizo ya kiakili kutokana na matumizi mabaya ya bangi kwa miaka mingi, OCPD wa Nyandarua Kaskazini Francis Mwangi alisema.

Hisia ziliongezeka katika kijiji cha Kwa-Soiro kilomita chache kutoka kituo cha biashara cha Njabini huko Kinangop baada ya mauaji hayo ya panga siku ya Jumamosi.

Saa chache baada ya kukamatwa, mshukiwa huyo alikuwa akipiga kelele na 'kuhubiri' katika kituo cha polisi cha Njabini. Polisi walimnukuu akisema dhamira yake ya kidunia imekamilika.

OCPD Mwangi alisema mkongwe huyo alitolewa nje ya nyumba yake, kisha kushambuliwa kwa panga.

"Mshukiwa alienda na kuripoti kisa hicho katika kituo cha polisi huku mwanamke huyo akikimbizwa katika Hospitali ya Kinangop Kaskazini ambako alitangazwa kuwa amefariki alipofika," alisema.

Wakati huo huo, watu watatu akiwemo mtoto mchanga walifariki kando ya barabara kuu ya Nairobi-Nakuru kufuatia ajali iliyohusisha gari la kibinafsi na trela.

Mama amelazwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Naivasha akiwa mahututi kufuatia ajali ya wikendi karibu na Marula Farm kilomita 10 kutoka mji wa Naivasha.

Dereva alikuwa akipita kundi la magari alipogongana uso kwa uso na trela na kusababisha kifo cha abiria wa kiume papo hapo.

Mtoto mchanga na dereva walikufa hospitalini. Waliokuwa kwenye trela hawajeruhiwa.

OCPD wa Naivasha Samuel Waweru alisema dereva wa gari la kibinafsi ndiye alaumiwa.

"Gari la kibinafsi lilikuwa likipita kundi la magari wakati lilipogonga trela na kuua dereva, abiria wa kiume na mtoto wa siku tano."