Ruto alipata Sh93.7m pekee kwenye hazina - Seneta Cherargei

Seneta huyo aliwaomba Wakenya kuwa na subira akisema suala hilo linashughulikiwa.

Muhtasari

•"Uchumi hauko tena ICU Bali Kifo kwa sababu H.E Ruto alipata Sh93.7M pekee kwenye hazina, Uhuru alienda nyumbani na kila kitu. State Capture ni kweli !" Cherargei alisema.

•Kaunti hazijapokea fedha kutoka kwa Hazina ya Kitaifa kwa muda wa miezi mitatu iliyopita.

Seneta wa Nandi Samson Cherargei
Image: MAKTABA

Seneta wa Kaunti ya Nandi Samson Cherargei amedai kuwa Rais William Ruto alipata Sh93.7 milioni pekee katika Hazina.

Katika taarifa yake Jumamosi kuhusu uchumi, Seneta huyo aliwaomba Wakenya kuwa na subira akisema suala hilo linashughulikiwa ili kurudisha nchi mahali ufaapo.

"Uchumi hauko tena ICU Bali Kifo kwa sababu H.E Ruto alipata Sh93.7M pekee kwenye hazina, Uhuru alienda nyumbani na kila kitu. State Capture ni kweli !" Cherargei alindika kwenye Twitter siku ya Jumamosi.

"Nchi ni fukara, Wakenya kuweni na subira H.E Ruto atarekebisha hili kupitia mageuzi ya kiuchumi na Maombi kutoka kwetu sote. Amina."

Haya yanajiri huku magavana wakisubiri agizo la serikali kuhusu kucheleweshwa kwa ufadhili wa kaunti.

Kaunti hazijapokea fedha kutoka kwa Hazina ya Kitaifa kwa muda wa miezi mitatu iliyopita.

Gavana wa Kisii Simba Arati alisema wana matumaini kuwa Ruto atatimiza ahadi yake kuhusu ufadhili na uhamisho wa majukumu kwa kaunti.

"Kaunti zinakodolea macho mgomo unaokaribia wa wafanyikazi kwa sababu walilipwa mara ya mwisho mnamo Julai. Magavana wapya hawana uhakika wa jinsi ya kukabiliana na hili. Tunatumai pesa hizo zitatolewa kwa wakati," Arati alisema.

Akiongea Jumanne wakati wa kuapishwa kwake, Ruto alisema ruzuku ya mafuta imetumia pesa nyingi zisizo za lazima.

"Katika ruzuku ya mafuta pekee, jumla ya Ksh144 bilioniza walipa kodi zimetumika , ambayo ni Ksh 60 bilioni katika kipindi cha miezi 4 iliyopita," alisema.

Alisema mpango huo hauwezekani endelevu huku akitangaza kusitishwa  kwa ruzuku hiyo.