Raila ataka Interpol kuongoza uchunguzi wa kifo cha wakili Paul Gicheru

Gicheru alishtakiwa katika Mahakama ya ICC kwa kuingilia mashahidi kuhusiana na kesi ya ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007-08.

Muhtasari

• Waziri Mkuu huyo wa zamani aliifariji familia ya Gicheru na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu ugonjwa wa mwana wao.

Raila Odinga
Image: RAILA ODINGA/TWITTER

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga amewataka polisi wa Kimataifa wa Interpol kuanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mshukiwa wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), wakili Paul Gicheru.

Katika taarifa iliotolewa na msemaji wa Raila Prof Makau Mutua mnamo Jumatano, Septemba 28, Raila alitaja kifo hicho kuwa cha kushangaza na kisichoelezeka.

"Mfano wa vifo vya ajabu na visivyoelezeka, vingine vikiwa vya kutisha na vibaya, ni vya kutatanisha sana.

Amesema kwamba ili kuzuia mauaji hayo kuzimwa, amewataka maafisa wa Interpol kuongoza Uchunguzi huo, ilisema Taarifa hiyo.

Raila alieleza kuwa kifo cha Gicheru kilikuwa na athari za kimataifa kwani ICC ilimweka kizuizini wakati wa kifo chake.

Alisema kuwa kwasababu ya kuwa mwanachama wa Mahakama hiyo yenye makao yake The Hague, Kenya haikuwa na chaguo ila kuruhusu uchunguzi.

Waziri Mkuu huyo wa zamani aliifariji familia ya Gicheru na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu ugonjwa wa mwana wao.

Gicheru alikuwa ameshtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa kuingilia mashahidi kuhusiana na kesi ya ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007-08, ambapo alikana mashtaka.