Majonzi! Wanafamila 7 wateketea hadi kufa Embu

Saba hao ni pamoja na mume, mke, watoto wao watatu na wajukuu wawili.

Muhtasari

•Naibu kamishna wa Kaunti Ndogo ya Embu Mashariki Jane Waruinge alisema mkasa huo ulitokea Jumapili asubuhi.

Wanafamilia saba walifariki hadi kufa katika mkasa wa moto Jumapili asubuhi.
Image: BENJAMIN NYAGA

Watu saba wamefariki katika kijiji cha Ngimari, kaunti ya  Embu baada ya moto kuteketeza nyumba yao hadi kuwa majivu Jumapili asubuhi.

Miongoni mwa waliopoteza maisha yao ni pamoja na mume, mke, watoto wao watatu na wajukuu wawili.

Akithibitisha kisa hicho, naibu kamishna wa Kaunti Ndogo ya Embu Mashariki Jane Waruinge alisema mkasa huo ulitokea Jumapili asubuhi.

 "Hatujatambua chanzo cha moto huo lakini tuna maafisa wetu wote katika eneo la tukio na uchunguzi unaendelea," alisema.

Mengine yanafuata...

Wakazi wa kijiji cha Ngimari wakusanyika katika eneo la tukio.
Image: BENJAMIN NYAGA