Huduma Center zaongezewa muda wa kuhudumu

Jumwa alisema Wakenya wanapaswa kutarajia mabadiliko katika siku 100 zijazo.

Muhtasari

• Wizara pia inapanga kuzindua kituo hivyo katika maeneo ya kaunti ndogo kwa ushirikiano na hazina ya NG-CDF.

Aliyekuwa mbunge wa Malindi Aisha
Aliyekuwa mbunge wa Malindi Aisha

Waziri wa Utumishi wa Umma, Jinsia na usawa Aisha Jumwa ametangaza kuongeza muda wa saa za kazi za vituo vya Huduma Centers .

Jumwa alisema vituo hivyo 18 vitafanya kazi kuanzia saa moja  asubuhi hadi saa moja jioni.

"Kulingana na haya, wizara imeanza kuongeza saa za kazi kwa zamu kwa Vituo vya Huduma Centers kutoka saa moja asubuhi hadi saa tatu jioni," alisema.

Wizara pia inapanga kuzindua kituo hivyo katika maeneo ya kaunti ndogo kwa ushirikiano na hazina ya NG-CDF, ili kelta huduma za serikali karibu na wananchi katika maeneo ya mashambani.

"Tutazindua huduma 100 za Huduma Mashinani kote nchini," alisema.

Jumwa alisema Wakenya wanapaswa kutarajia mabadiliko katika siku 100 zijazo.

Waziri alisema ananuia kuzindua mpango ulioboreshwa wa mafunzo kuhusu Viwango vya Huduma Kenya na Ubora wa Huduma kwa Wateja ili kuwapa wafanyakazi ujuzi unaohitajika kuwahudumia wateja vyema.

"Kama sehemu ya maagizo ya ya rais, tunapanga pia kuzindua mpango wa upandaji miti kupitia Huduma Center inayolenga kupanda miti milioni 500 katika miaka mitano ijayo," alisema.