Jumba la ghorofa 8 la poromoka Tasia,Embakasi

Jengo hilo lilikuwa na biashara katika ghorofa ya chini.

Muhtasari
  • Mnamo Septemba, watu wawili waliaga dunia na saba kuokolewa baada ya nyumba ya ghorofa sita iliyokuwa ikijengwa kuporomoka katika eneo la Kirigiti, Kaunti ya Kiambu

Jengo la ghorofa nane limeporomoka Kwa-Ndege, Tassia, Embakasi.

Kikosi cha uokoaji kutoka Msalaba Mwekundu kwa sasa kiko kwenye eneo la tukio kwa uokoaji.

Kulingana na nduru za habari ghorofa ya chini na ghorofa ya kwanza ya jengo hilo iliathirika pakubwa.

"Jengo lilipoanza kuporomoka, watu walihama," shahidi aliambia vyombo vya habari.

Hakuna majeruhi walioripotiwa kufikia sasa.

Jengo hilo lilikuwa na biashara katika ghorofa ya chini.

Mnamo Septemba, watu wawili waliaga dunia na saba kuokolewa baada ya nyumba ya ghorofa sita iliyokuwa ikijengwa kuporomoka katika eneo la Kirigiti, Kaunti ya Kiambu.