logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mshukiwa wa 3 wa mauaji ya mfanyibiashara wa Kiambu Mwangi atiwa mbaroni

Mwangi alikuwa amefanya kazi katika nyumba hiyo kwa miaka minne

image
na Radio Jambo

Habari07 November 2022 - 12:00

Muhtasari


  • Wachunguzi wanaamini kuwa marehemu, ambaye alirejea Kenya kutoka Kigali mnamo Septemba 13, 2022, aliuawa kwa madai ya kuwa na uhusiano na Lucy Muthoni

Mshukiwa wa tatu anayedaiwa kuhusika katika mauaji ya kutisha ya mfanyabiashara George Mwangi Kamau amekamatwa.

Wapelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) wanamzuilia John Muikiriria Mwangi, ambaye inasemekana alitoweka siku moja kabla ya marehemu kuuawa, huko Karinga kaunti ndogo ya Gatundu Kusini.

Kulingana na DCI, kutoweka kwake kulizua uvumi kuhusu ni kwa nini alitoweka kwa njia isiyoeleweka siku hiyo hiyo mshukiwa wa pili, Morris Mbugua, alipoajiriwa na Gladys Njeri Mwangi almaarufu Chania, ambaye ni mshukiwa mkuu na mke wa marehemu.

Mwangi alikuwa amefanya kazi katika nyumba hiyo kwa miaka minne na alionekana mara ya mwisho Chania alipomtuma kuweka pesa kwenye duka la M-pesa.

"Wapelelezi hao mahiri waligundua kuwa ni sadfa kwamba mshtakiwa wa pili Morris Kamau Mbugua aliajiriwa Oktoba 8, 2022 na mshukiwa mkuu Gladys Njeri Mwangi, siku moja kabla ya kifo na kutoweka kwa marehemu, John Muikiriria Mwangi, alipotea siku hiyo hiyo,” taarifa ya  DCI kwenye Twitter ilisoma.

Wachunguzi wanaamini kuwa marehemu, ambaye alirejea Kenya kutoka Kigali mnamo Septemba 13, 2022, aliuawa kwa madai ya kuwa na uhusiano na Lucy Muthoni.

Mwili wa mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 58 ulipatikana katika msitu wa Kieni, Kaunti ya Kiambu, Oktoba 12, saa chache kabla ya kudaiwa  kurejea nchini.

Mwili huo uligunduliwa ukiwa umefungwa kwenye mfuko wa nailoni na kuzikwa chini ya rundo la katoni.

Kulingana na DCI, Chania aliripoti kutoweka kwa mumewe mnamo Oktoba 11, 2022, katika Kituo cha Polisi cha Mwea, Gatundu Kaskazini.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved