logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ajali ya ndege Ziwa Victoria: Ufaransa yatuma maafisa kuchunguza chanzo cha ajali

Wataalamu hao waliwasili jioni ya jana Jumanne.

image
na Radio Jambo

Makala09 November 2022 - 06:11

Muhtasari


•Ufaransa imetangaza kutuma kikosi cha wataalamu wa uchunguzi na uchambuzi wa masuala ya usalama wa ndege kusaidia uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Precision Air .

Serikali ya Ufaransa kupitia ubalozi wake jijini Dar Es Salaam imetangaza kutuma kikosi cha maafisa na wataalamu wa uchunguzi na uchambuzi wa masuala ya usalama wa ndege kusaidia uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Precision Air iliyoanguka Jumapili mjini Bukoba na kuua watu 19 hukuwengine 24 wakiokolewa.

Taarifa ya kutumwa kwa kikosi hicho imetolewa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui. Wataalamu hao waliwasili jioni ya jana Jumanne.

Ndege iliyopata ajali imetengenezwa na kampuni ya ATR ambayo inamilikiwa na makampuni mawili makubwa ambayo ni AIRBUS kutoka Ufaransa na LEONARDO kutoka Italia.

Kampuni ya ATR pia imetuma wataalamu wake nchini Tanzania kusaidia uchunguzi kama inavyotakiwa na sheria za kimataifa za usalama wa anga.

Mamlaka za Tanzania awali zilitangaza kuwa hali ya hewa mjini Bukoba ilikuwa mbaya wakati ajali hiyo ikitokea.

Uchunguzi wa kina ulianzishwa toka Jumapili na Serikali ya Tanzania na sasa timu hizo za wataalamu kutoka ng’ambo zinatarajiwa kuupa kasi uchunguzi huo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved