Hongereni-Raila awapongeza wabunge wa EALA kutoka Azimio

Kennedy alizoa kura 262 akifuatiwa na Winnie aliyepata kura 247, Kega (197) na Shahbal (181).

Muhtasari
  • Muungano huo utawakilishwa na Kennedy Kalonzo, Winnie Odinga, aliyekuwa mbunge wa Kieni Kanini Kega na mfanyibiashara Suleiman Shahbal
WABUNGE WA EALA KUTOKA AZIMIO KUTOKA KUSHOTO:SULEIMAN SHAHBAL,KANINI KEGA,WINNIE ODINGA NA KENNEDY KALONZO
Image: TWITTER/RAILA ODINGA

inara wa Azimio Raila Odinga amewapongeza viongozi wanne waliochaguliwa kuwakilisha Kenya katika Bunge la Afrika Mashariki.

Muungano huo utawakilishwa na Kennedy Kalonzo, Winnie Odinga, aliyekuwa mbunge wa Kieni Kanini Kega na mfanyibiashara Suleiman Shahbal.

Katika taarifa yake Ijumaa, Raila aliwapongeza akisema watatimiza tamko la Azimio la EAC. "

Tamko la Azimio lilitolewa Arusha na Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1976. Tunajivunia kwamba leo muungano wa Azimio La Umoja One Kenya unatuma wabunge wake Arusha kutimiza Azimio la Azimio la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hongereni sana!" Alisema.

Kennedy alizoa kura 262 akifuatiwa na Winnie aliyepata kura 247, Kega (197) na Shahbal (181).