• Watahiniwa wa gredi ya 6 na darasa la nane wataanza mitihani yao Novemba 28.
• Wanafuzi wa kidato cha nne wataanza KCSE mnamo Desemba 02, 2022.
Wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari zinafungwa rasmi Ijumaa Novemba 25 kwa likizo ndefu ya wiki nane.
Wanafunzi wanatarajiwa kufunga shule hili kuwapa nafasi watahiniwa wa mitihani ya kitaifa kufanya mtihani wao wa CBC wa gredi ya 6, KCPE wa darasa la nane, na KCSE kwa wanafunzi wa kidato cha 4 unaotarajiwa kuanza wiki ijayo.
Wanafunzi wa gredi ya 6 na darasa la nane wanataanza mtihani wao mnamo Novemba 28 hadi Novemba 30.
Watahiniwa wa kidato cha nne wanatarajiwa kuanza siku ya Alhamisi Desemba 02, 2022 na kumaliza tarehe 23 Desemba 2022.
Mbali na hayo wazazi wamelilia kuongezeka kwa karo ya shule ambayo ni pigo kubwa kwao kwani ni mzigo mkubwa kwao.
Haya yamejiri baada ya serikali kuondoa ruzuku iliyokuwa inawasaidia wazazi kulipa karo kidogo ila sasa ni pigo kwa wazazi maana karo itapanda kwanzia mwaka ujao.