4G CAPITAL

Tunawasherehekea Mashujaa wa Hustle na 4G Capital

4G Capital imesaidia biashara ndogo ndogo barani Afrika tangu 2013.

Muhtasari
  • Mashujaa wa Hustle ni nani? Ni watu ambao wanaendelea kusonga mbele hata nyakati zinapokuwa ngumu.
  • Wanawake wawili wamesimulia hadithi zao za mafanikio kwa 4G Capital na kueleza jinsi huduma hiyo imekuwa na jukumu muhimu katika ukuaji wa biashara zao.

Mashujaa wa Hustle ni nani? Ni watu ambao wanaendelea kusonga mbele hata nyakati zinapokuwa ngumu. Ni watu ambao wanaweza kujikwaa lakini wakasimama tena. Wao ni msukumo. Je, wewe ni mwanamke anayefanya kazi katika sekta isiyo rasmi? Kwetu sisi, nyinyi ndio #MashujaaWaHustle.

Iwe wewe ni kijana hustler unayejaribu kukuza saluni yako, kibanda cha chakula, biashara ya samani au hata kibanda cha matunda. Tunakusherehekea leo na kutambua hatua zote ambazo umechukua kwa mafanikio ya biashara yako.

Wanawake wawili wamesimulia hadithi zao za mafanikio kwa 4G Capital na kueleza jinsi huduma hiyo imekuwa na jukumu muhimu katika ukuaji wa biashara zao.

Jane Nginyo, mfugaji wa kuku, amefanya uwekezaji mkubwa katika shamba lake la kuku kutumia mikopo ya biashara ya 4G Capital. Amefanikiwa kukuza ukubwa wa shamba lake kwa asilimia 500 (kutoka kuku 200 hadi 1000) kwa muda wa miaka 4.  Amechukua jumla ya mikopo 31 ya 4G Capital  na sasa anaendesha biashara yenye faida kubwa. Ameweka akiba ya kutosha kununua gari la kuleta mayai sokoni na pia kuwasomesha watoto wake.

Mary Wanjiru Maina, mwokaji mikate, alianza safari yake akiwa na kijiko cha mbao na tanuri ndogo ya makaa, akioka kilo 2 tu za unga kwa siku. Kwa kuwa hakuwa na akiba ya kibinafsi ya kuwekeza katika biashara yake, na hakuweza kukidhi mahitaji ya benki kwa ajili ya mikopo ya biashara, Mary alikosa njia ya kupanua duka lake ili kukidhi mahitaji ya ndani.

Amechukua jumla ya mikopo 35  kutoka kwa 4G capital na kufikia sasa amewekeza kwenye mashine ya kuchanganya, oveni mbili za umeme na sasa anaoka kilo 120 za unga kwa siku. Wauzaji huchukua bidhaa zake kila siku na kusambaza kwa maduka, hivyo basi kuongeza idadi ya wateja wake.

Kama tu Jane na Mary, kujisajili na 4G Capital kunaweza kuwa hatua sahihi kwa biashara yako.

4G Capital imesaidia biashara ndogo ndogo barani Afrika tangu 2013, ikitoa mafunzo ya ujuzi wa kifedha na mikopo ya mitaji ili kusaidia biashara ndogo ndogo kukua kwa uendelevu.

Mkopo wa UPIA ni mkopo wao mzuri wa siku 30 ambao umeundwa kukusaidia kukuza biashara yako. Hauna dhamana, ni wa Faragha, wa papo hapo, ni wa bei nafuu na utafikiwa na mkopo ndani ya saa 24 baada ya kuidhinishwa.

Umesikia kuhusu loan yetu ya UPIA? Tupigie kwa 0111113001 au 0758693269 ndio tuwasiliane zaidi. #4Growth #4Good

Posted by 4G Capital Kenya on Wednesday, October 12, 2022

Zaidi ya hayo, tofauti na programu zingine za mkopo wa simu, 4G Capital haifichui maelezo yako ya mkopo kwa marafiki au jamaa zako.

4G Capital pia imezindua mpango wa uaminifu kwa wateja ambapo wateja wamepangwa katika makundi kuanzia Bronze, Silver, Gold na Diamond. Hii inatokana na jinsi unavyorejesha mkopo.  Kadri unavyopanda, ndivyo kiwango cha riba kinavyopungua.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kukuza biashara yako ukitumia 4G Capital, wapigie sasa kwa 0111113001 au piga *612# ili kujisajili.