Ruto ateua jopo kuchunguza walioteuliwa na NPSC

Haya yalitangazwa kupitia notisi maalum ya Gazeti iliyoshirikiwa na Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed ya Alhamisi, Januari 12.

Muhtasari
  • "Majopo yataajiri watakaochukua nafasi za Priscilla Nyokabi (NGEC) na Naftali Rono (NPSC)," Mohamed alisema.
RAIS WILLIAM RUTO

Rais William Ruto aliteua kamati ya watu saba kuwahoji walioteuliwa  kuwa wanachama wa Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi (NPSC).

Haya yalitangazwa kupitia notisi maalum ya Gazeti iliyoshirikiwa na Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed ya Alhamisi, Januari 12.

"Majopo yataajiri watakaochukua nafasi za Priscilla Nyokabi (NGEC) na Naftali Rono (NPSC)," Mohamed alisema.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya uteuzi ni pamoja na Arthur A. Osiya, Joyce Nyabuti, Gilbert Chabari Mutembei, Monica Muiru, Raymond Plal Sangsang Nyeris, Joyce M. Mutinda, na Mbeti Mchuki.

"Katika kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na kifungu cha sita (1)(a) cha Sheria ya Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi, 2011, mimi William Samoei Ruto, Rais na Kamanda- Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya ateue waliotajwa hapo juu," ilisema sehemu ya notisi hiyo.

NPSC ina jukumu la kusimamia rasilimali watu katika Huduma ya Polisi, ambayo hapo awali ilikuwa ikishughulikiwa na Tume ya Utumishi wa Umma.