KCPE 2022: Fahamu jinsi mtahiniwa anaweza kujua shule ya sekondari ambayo ameitwa

Huduma hiyo ya SMS inapatikana kwa huduma yoyote ya simu.

Muhtasari

•Machogu aliwataka wazazi kutuma index number za watahiniwa kwa 22263 ili kujua watoto wao wamechaguliwa shule gani.

•Watahiniwa wanaweza pia kuangalia kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu ili kupata maelezo ya uteuzi wa Kidato cha Kwanza.

Watahiniwa wa darasa la nane wakalia mtihani wa KCPE
Watahiniwa wa darasa la nane wakalia mtihani wa KCPE
Image: MAKTABA

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu ametangaza kuwa watahiniwa waliofanya mtihani wao wa KCPE wa 2022 wamechaguliwa kujiunga na shule mbalimbali za upili.

Machogu aliwataka wazazi kutuma index number za watahiniwa kwa 22263 ili kujua watoto wao wamechaguliwa shule gani.

Huduma hiyo ya SMS inapatikana kwa huduma yoyote ya simu na itatozwa Sh25 kila moja.

Watahiniwa wanaweza pia kuangalia kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu ili kupata maelezo ya uteuzi wa Kidato cha Kwanza.

Jumla ya watahiniwa 1,244,188 walisajiliwa kufanya KCPE katika vituo 493 vya kuhifadhi na kusambaza mitihani.

Machogu alitoa matokeo ya Cheti cha Elimu ya Msingi cha 2022 (KCPE) mnamo Desemba 21, 2022.

Alisema atahakikisha mpito wa asilimia 100 hadi sekondari.

Waziri huyo aliwaonya wazazi kutowaweka watoto wao nyumbani wakati wa kujiunga na kidato cha kwanza.

"Watahiniwa wote ambao matokeo yao ninatoa leo watakubaliwa katika kidato cha 1 chini ya sera ya mpito ya asilimia 100," alisema.

Hili lilikuwa toleo la pili la mwisho la mtihani wa KCPE kabla ya mfumo wa elimu wa 8-4-4 kuondolewa kabisa katika mtaala wa shule za msingi mwaka ujao.

Ni mara ya kwanza Machogu kusimamia uteuzi wa watahiniwa katika shule ya upili.