Kisii:Walimu sita wakamatwa kwa kuwalazimisha wanafunzi kufanya vitendo vichafu

Kulingana na polisi, sita; Everline Moraa, Gladys Kenyanya, Angelicia Joseph, Moraa Nyairo, Cathrine Mokaya na William Isoka,

Muhtasari
  • Katika video hiyo ambayo imezua hisia mseto mitandaoni wavulana hao wadogo waliovalia sare za shule wanalazimishwa na walimu wao kufanya kitendo kichafu
Picha: KWA HISANI
Picha: KWA HISANI

Walimu sita kutoka Kaunti ya Kisii wamekamatwa kutokana na video ya kutatanisha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo watoto wa shule wananaswa wakionyeshwa kitendo kichafu.

Akithibitisha kukamatwa kwa walimu hao watano wa kike na mmoja wa kiume, OCPD wa Nyamache Kipkulei Kipkemboi alisema kisa hicho kilitokea katika Shule ya Msingi ya Itumbe DOK huko Nyamache.

Kulingana na polisi, sita; Everline Moraa, Gladys Kenyanya, Angelicia Joseph, Moraa Nyairo, Cathrine Mokaya na William Isoka, walikamatwa baada ya maafisa wa Wizara ya Elimu katika kaunti hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kaunti Ndogo ya Nyamache Linet Onduso kuzuru shule hiyo baada ya kupokea klipu hiyo.

Katika video hiyo ambayo imezua hisia mseto mitandaoni wavulana hao wadogo waliovalia sare za shule wanalazimishwa na walimu wao kufanya kitendo kichafu huku wakiwa wamelala juu ya kila mmoja huku walimu wakicheka kwa sauti ya chini.

Kulingana na OCPD, walimu hao sita wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Nyamache wakisubiri kufikishwa mahakamani.