Tanzia:Aliyekuwa mkewe waziri Ababu Namwamba aaga dunia

Familia ilisema kwamba Mwaro amepitia mengi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Muhtasari
  • Kulingana na familia yake, Marehemu alikuwa amesherehekea siku yake ya kuzaliwa siku ya Jumanne, Machi 7, saa chache kabla ya kifo chake cha ghafla.
  • Mwili wake unasemekana kuhamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha MP Shah jijini Nairobi

Priscah Mwaro, aliyekuwa mke wa Waziri wa Michezo na Sanaa Ababu Namwamba amefariki jijini Nairobi.

Kifo chake kilithibitishwa na jamaa zake wa karibu, ambao hawakufichua maelezo zaidi.

Mwili wake unasemekana kuhamishiwa chumba cha kuhifadhi maiti cha MP Shah jijini Nairobi.

Priscah alikuwa mke wa Ababu kwa miaka mitatu, na kubarikiwa watoto watatu. Wawili hao walikosana na kutengana.

Kulingana na familia yake, marehemu alikuwa amesherehekea siku yake ya kuzaliwa siku ya Jumanne, Machi 7, saa chache kabla ya kifo chake cha ghafla.

Aidha, familia ilisema kwamba Mwaro amepitia mengi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Kutoka kwetu hapa Radio Jambo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.