Tutaheshimu uamuzi wa mahakama kuhusu kesi ya Matiang'i - Kindiki

Kindiki, alipokuwa akihutubia wanahabari siku ya Jumatano, alisema sera ya serikali itahusisha kuheshimu kabisa utawala wa sheria.

Muhtasari
  • Alisema kuzingatiwa kwa vyombo vyote vya kikatiba na heshima kwa afisi zote huru za Kenya kutazingatiwa
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KITHURE KINDIKI
Image: KWA HISANI

Waziri wa Mambo ya Ndani Kindiki Kithure amesema serikali itaheshimu uamuzi wowote ambao Kurugenzi ya Uchunguzi wa Jinai itatoa kuhusu kesi ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i.

Kindiki, alipokuwa akihutubia wanahabari siku ya Jumatano, alisema sera ya serikali itahusisha kuheshimu kabisa utawala wa sheria.

Alisema kuzingatiwa kwa vyombo vyote vya kikatiba na heshima kwa afisi zote huru za Kenya kutazingatiwa.

"Ingawa ninapongeza ustadi wa polisi katika kushughulikia suala la Dkt Matiang’i, serikali itaheshimu maamuzi yaliyofikiwa na DCI," akasema.

Alisema DCI tayari imekamilisha uchunguzi wao kuhusu kesi hiyo na mapendekezo yaliyowasilishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma

"Serikali itaheshimu kwa usawa uhuru wa uamuzi wa DPP na iwapo mtu yeyote atafunguliwa mashtaka kutokana na uchunguzi huu; serikali itaheshimu matokeo na uamuzi wa mahakama,” aliviambia vyombo vya habari.

Siku ya Jumanne, Matiang'i akiwa na mawakili wake alifika mbele ya afisi za DCI kuhoji kuhusu madai ya kuchapishwa kwa taarifa za uongo.