Mwanamume,60, ajiua baada ya mkewe kudaiwa kuwa na uhusiano na mwanamume wa miaka 24

Mke aliripotiwa kutibiwa na kuruhusiwa. Hata alitangulia kuandikisha ripoti katika Kituo cha Polisi cha Wang'uru.

Muhtasari
  • Chifu Kariuki alisema kuwa mwanamume huyo aliyeonekana kuwa na mkazo kuhusu uchumba huo alikuwa ameazimia kumwacha mkewe.
Kitanzi
Kitanzi
Image: HISANI

Mzee wa miaka 60 huko Mwea, Kaunti ya Kirinyaga amefariki kwa kujitoa mhanga baada ya kudaiwa kugundua mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Mwili wake ulipatikana ukining’inia kwenye paa huku akiwa amefungwa kamba shingoni.

Henry Kariuki, Chifu wa Kijiji cha Kiarukungu, alifichua kuwa marehemu alizuru afisi yake Jumatano akielezea kutamaushwa kuhusu uhusiano wa nje wa ndoa wa mkewe.

Baadaye alifahamishwa kuhusu kisa ambapo mwanamume mmoja alimvamia mkewe kwa panga, ndipo akagundua kuwa ni marehemu ndiye aliyefanya kitendo hicho.

Mke aliripotiwa kutibiwa na kuruhusiwa. Hata alitangulia kuandikisha ripoti katika Kituo cha Polisi cha Wang'uru.

Chifu Kariuki alisema kuwa mwanamume huyo aliyeonekana kuwa na mkazo kuhusu uchumba huo alikuwa ameazimia kumwacha mkewe.

Ripoti zinaonyesha kuwa mwanamke huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni mchuuzi wa nyanya kijijini hapo.

“Hatukufikiri kwamba mambo yangeisha hivi kwa sababu alikuwa amesema ameamua kuwaacha wawili hao wafanye walivyotaka,” chifu huyo aliongeza.

Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Mwea Mashariki Daniel Kitavi alithibitisha kisa hicho, akisema marehemu alitakiwa kufika kituoni kurekodi taarifa na kupatikana amefariki.