Rais William Ruto amewateua Makatibu Wakuu 50 kuhudumu katika serikali yake. Hii ni baada ya kufanikiwa kupitia mahojiano makali yaliyofanywa na Tume ya Utumishi wa Umma.
Wateule hao sasa watahakikiwa na Bunge kabla ya kuteuliwa na Rais. Ann Mwangi, Nicholas Rioba na Edwin Wandambusi wameteuliwa kuhudumu katika afisi ya Naibu Rais.
Aliyekuwa Mbunge wa Kuteuliwa Isaac Mwaura, Sharif Ali na Rehema Hassan baada ya kuidhinishwa na bunge watahudumu katika afisi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri.
Aliyekuwa Seneta Aliyeteuliwa Millicent Omanga sasa atahudumu kama CAS katika Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa pamoja na Mohamud Ali na Samuel Tunai.
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Evans Kidero atahudumu katika Wizara ya Uwekezaji na Biashara, pamoja na Lilian Tomitom na Vincent Mogakarodha Kamili Ofisi ya Naibu Rais
Orodha kamili ya CAS.
Wizara ya Ulinzi.
Alfred Agoi Masadia.
Hazina ya Kitaifa na Mipango ya Kiuchumi .
Kirui Joseph Limo na Beatrice Nkatha Nyaga.
Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora.
Joash Arthur Maangi Catherine Waruguru.
Wizara ya Utumishi wa Umma, Jinsia & Hatua za Upendeleo.
Hussein Tuneya Dado na Charity Nancy Nanyama Kibaba.
Wizara ya Barabara na Uchukuzi.
Benjamin Jomo na Washiali Nicholas Gumbo.
Wizara ya Ardhi, Kazi za Umma, Nyumba na Maendeleo ya Miji.
Onesmus Kimani Ngunjiri na Victor Kioko Munyaka.
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali.
Denis Njue Itumbi na Simon Mwangi Kamau
Wizara ya Afya
James Kimanthi Mbaluka na Khatib Abdallah Mwashetani.
Wizara ya Elimu.
Elly Stephen Loldepe.
Mark Lomunokol Anab.
Mohamed Gure.
Wizara ya Kilimo Maendeleo ya Mifugo.
Jackson Kiptanui na Daniel Wamahiu Kiongo.
Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda.
Evans Odhiambo Kidero.
Vincent Kemosi Mogaka.
Lilian Cheptoo Tomitom.
Wizara ya Ushirika na Maendeleo ya Biashara Ndogo, Ndogo na za Kati (MSMEs) (Askofu) .
Margaret Wanjiru na Amos Chege Mugo
Wizara ya Mambo ya Vijana, Sanaa na Michezo .
Wesley Korir na Charles Njagua Kanyi.
Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu .
Jackline Mwenesi na Lukalo Nyaga John Muchiri.
Wizara ya Utalii, Wanyamapori na Urithi.
Wilson Sossion na Rehema Dida Jaldesa.
Wizara ya Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji.
Chrisantus Wamalwa na Sunya Orre.
Wizara ya kawi na Petroli.
Mary Yaine Seneta na John Lodepe Nakara.
Wizara ya Kazi na Ulinzi wa Jamii.
Elijah Gitonga Rintaugu.
Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ASLS & Maendeleo ya Kikanda.
Mwanamaka Amani Mabruki na Rael Chebichii Lelei.
Wizara ya Madini, Uchumi wa Bluu na Masuala ya Bahari.
David Kipkorir Kiplagat Fredrick Otieno Outa.
Ofisi ya Sheria ya Jimbo.
Allan Kibet Kosgey.