Tutamshtaki Ruto ICC kwa kuvunja sheria-Raila asema

Wabunge hao walikamatwa mapema JUmatatu, wakiwa kwenye maandamano eneo la KICC Nairobi.

Muhtasari
  • Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo pamoja na wabunge Amina Mnyazi na Ken Chonga wanazuiliwa.

Kiongozi wa Azimio akihutubia Wakenya kwenye maandamano siku ya Jumatatu amekiri kwamba atamshtaki Rais Ruto kwa kuvunja sheria

Raila alisema haya huku akikashifu kukamatwa kwa baadhi ya wabunge wa mrengo wa Azimio.

Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo pamoja na wabunge Amina Mnyazi na Ken Chonga wanazuiliwa.

Wabunge hao walikamatwa mapema JUmatatu, wakiwa kwenye maandamano eneo la KICC Nairobi.

"Bwana Ruto anawatuma maafisa wa polisi kuwakamata wanasiasa wetu, tutamshtaki huko ICC kwa kuvunja sheria

Wameshikwa na uoga lakini mambo bado. Leo ni kionjo tutaendelea mpaka tufike kule tunaelekea. Mpaka bei ya unga, mafuta na chakula irudi chini alafu baadae tupate haki yetu ya uchaguzi,"Raila amesema.

Polisi wamerusha vitoa machozi msafara wa magari yaliyokuwa yamembeba kiongozi wa upinzani Raila Odinga na wanasiasa wengine, vyombo vya habari vya nchini vimeripoti.

Walioandamana na kiongozi huyo ni pamoja na;Martha Karua,Junet Mohamed,Kalonzo Musyoka, Gladys Wanga,Wajackoyah miongoni mwa viongozi wengine wa mrengo wa Azimio.

Kalonzo pia alimtaka Ruto kuachiliwa wabunge waliokamatwa mapema Jumatatu, huku akisema kwamba amevunja katiba.