logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Waandamanaji wawili wapigwa risasi wakivamia kituo cha polisi Migori

Maandamano makubwa yalishuhudiwa katika maeneo ambayo Ruto alitembelea Migori.

image
na

Habari27 March 2023 - 12:06

Muhtasari


•Watu wawili walipata majeraha ya risasi huku maandamano dhidi ya serikali yakishuhudiwa katika kaunti ya Migori.

•Waandamanaji waliokuwa na hasira waliimba nyimbo dhidi ya Mbunge Abuor wakimwita msaliti na kuchoma sanamu zake.

Waandamanaji wanaoipinga serikali wafunga daraja la mji wa Migori lililokuwa na shughuli nyingi na kuzuia msongamano wa magari mpakani mwa Kenya na Tanzania wiki jana. Wakiwa wamebeba sufuria tupu na vijiti vya kupikia, maandamano hayo yalitaka gharama kubwa za maisha kukabiliwa.

Watu wawili walipata majeraha ya risasi huku maandamano dhidi ya serikali yakishuhudiwa katika kaunti ya Migori, katika maeneo ambayo Rais William Ruto alitembelea siku ya Jumamosi.

Rais alitembelea mji wa Uriri na kituo cha Nyarach katika eneo bunge la Rongo yanayosimamiwa na wabunge waasi wa ODM Mark Nyamita(Uriri) na Paul Abuor(Rongo).

Shida ilianza Rongo huku waandamanaji waliokuwa na hasira wakikusanyika katika kituo cha Nyarach, ambako Ruto alikaribishwa na kuanza maombi maalum ya kusafisha eneo hilo kabla ya polisi kuwakamata waandamanaji kadhaa.

"Waandamanaji walipoenda katika kituo cha polisi cha Kamagambo kutaka mwenzao aachiliwe, polisi walifyatulia risasi umati ambapo wengine walijeruhiwa," Jackson Otiang'a, mkazi alisema.

Waandamanaji waliokuwa na hasira waliimba nyimbo dhidi ya Mbunge Abuor wakimwita msaliti na kuchoma sanamu zake.

Katika eneo la Uriri polisi, waliokuwa wamejihami walikuwa katika hali ya tahadhari huku vijana waliokuwa na hasira wakiwa wamebeba mabango na matawi wakiimba dhidi ya mbunge wao Nyamita na rais William Ruto wakiwashutumu kwa gharama ya juu ya maisha.

Kundi hilo liliimba “Nyamita Lazima aende!” "Ruto lazima aende!" huku wakizunguka eneo la mkutano wa Jumamosi.

Wakati maandamano katika mji wa Migori na maeneo mengine yakiwa ya amani, vituo hivyo viwili vilishuhudia vurugu huku polisi wakilazimika kufyatua risasi hewani na kuwarushia vitoa machozi waandamanaji waliokuwa na hasira.

“Tulikuwa na angalau wagonjwa wawili waliolazwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Rongo wakiwa na majeraha ya risasi. Mmoja bado alikuwa na risasi kwenye mguu," Maurice Otieno, msimamizi wa matibabu wa hospitali hiyo alisema.

Otieno alisema kuwa wawili hao walipokea matibabu ya huduma ya kwanza na walipewa rufaa katika Hospitali ya Rufaa ya Migori.

Kulikuwa na hofu kuwa idadi ya walioathirika ilikuwa sita huku wengine wakiripotiwa kupelekwa katika hospitali ya karibu ya Rosewood mjini Rongo.

Kamanda wa polisi wa Migori Mark Wanjala aliambia wanahabari kuwa hakufahamu kisa hicho.

Wiki iliyopita Jumatatu wakati wa maandamano kama hayo video ya wafuasi wa Nyamita na wale wa Azimio wakizozana ilienea kwenye mitandao ya kijamii.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved