7 wafariki katika maporomoko ya ardhi Gilgil

Saba hao wanawake watatu na watoto wanne walifariki baada ya kusombwa na tope kutoka kwa vilima vya Eburru Mbaruku

Muhtasari

• Mashirika ya kutoa misaada yakiongozwa na shirika Msalaba mwekundu yameanzisha shughuli ya kuwasaidia waathiriwa.

HELL'S GATE : Polisi wakiwa wamebeba moja ya miili iliyoopolewa kwenye korongo katika Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate, ambapo watu saba walikufa maji waliposombwa na mafuriko. Picha: FILE
HELL'S GATE : Polisi wakiwa wamebeba moja ya miili iliyoopolewa kwenye korongo katika Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate, ambapo watu saba walikufa maji waliposombwa na mafuriko. Picha: FILE

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali nchini imeendelea kusababisha maafa huku watu saba wakiaga dunia kutokana na maporomoko ya ardhi katika eneo la Gilgil.  

Saba hao wanawake watatu na watoto wanne walifariki baada ya kusombwa na tope kutoka kwa vilima vya Eburru Mbaruku katika kijiji cha Ol Jorai huko Eburru Mbaruk, Kaunti Ndogo ya Gilgil jana usiku. 

Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Gilgil Francis Tumbo alisema kuwa maporomoko hayo ya udongo yalisomba kijiji na kung'oa nyumba na majengo yaliyokuwa katika mkondo wake na hivyo kusababisha vifo vya watoto wanne na watu wazima watatu. 

Mashirika ya kutoa misaada yakiongozwa na shirika Msalaba mwekundu yameanzisha shughuli ya kuwasaidia waathiriwa.