IG Koome akiri kuchunguzwa kwa polisi aliyeshambulia wanahabari

"Tumepokea malalamiko hayo na yanashughulikiwa tuvumilie na tupeni muda," Koome alisema.

Muhtasari

• IG Koome aliwahakikishia wanahabari kuwa katika uongozi wake atahakikisha kuna uhusiano bora baina ya polisi na wahabari.

• Mkuu huyo wa polisi aliwaomba msamaha wanahabari waliojeruhiwa akisema kwamba haikuwa nia ya polisi kuwadhuru wanahabari bali ilikuwa ajali tu. 

• Koome alikiri kupokea taarifa za kujeruhiwa kwa baadhi ya waandishi wa habari wakati wakiripoti maandamano hayo.

Inspekta Jenerali aita mkutano wacdharura kujadili mbinu za kuzima maandamano ya Azimio
Inspekta Jenerali aita mkutano wacdharura kujadili mbinu za kuzima maandamano ya Azimio
Image: Maktaba

Inspekta Jenerali wa polisi Japhet Koome amewaomba radhi wanahabari kufuatia tukio ambapo polisi waliwashambulia wanahabari wakati ya maandamano yalioitishwa na muungano wa Azimio la Umoja.

Koome amefichua kuwa tayari uchunguzi umeanzishwa dhidi ya  afisa wa polisi aliyeonekane kwenye video akivunja vioo vya gari moja na kufyatua ndani gesi ya kutoa machozi.

Alisema ikiwa afisa yeyote wa polisi atapatikana na hatia ya kukuika sheria atachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo wa polisi aliwaomba msamaha wanahabari waliojeruhiwa akisema kwamba haikuwa nia ya polisi kuwadhuru wanahabari bali ilikuwa ajali tu. 

Aliwahakikishia wanahabari kuwa katika uongozi wake atahakikisha kuna uhusiano bora baina ya polisi na wahabari.

 "Nataka kuwahakikishia marafiki zetu kutoka kwa vyombo vya habari kwamba mashambulizi hayakuelekezwa kwao kwa makusudi. Tutaendelea kufanya kazi nanyi kwa karibu tunapopanga kuwajumuisha katika baadhi ya operesheni zetu zijazo," alisema.

Akizungumza siku ya Jumanne, Koome alipongeza Upinzani kwa kusitisha maandamano akisema polisi sasa watashiriki katika kuzuia uhalifu.

Alizungumza wakati wa mahojiano ya maafisa 12 wa polisi walioteuliwa kwa nafasi ya Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi katika Shule mafunzo ya Serikali ya Kenya.

Koome alikiri kupokea taarifa za kujeruhiwa kwa baadhi ya waandishi wa habari wakati wakiripoti maandamano hayo.

 "Tumepokea malalamiko hayo na yanashughulikiwa tuvumilie na tupeni muda," alisema.

Wadau katika sekta ya habari na mashirika ya haki za kibinadamu walishutumu mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari wakisema kuwa kuna hujumu uhuru wa vyombo vya habari.