Mwanamume akamatwa kwa madai ya kumnajisi bintiye wa miaka 2

Charity Wambui, mkazi alisema alishtuka kwani hajawahi kusikia kisa kama hicho katika kijiji hicho.

Muhtasari
  • Chifu wa eneo hilo Henry Karuki alisema mshukiwa huyo inasemekana alinaswa Jumatatu na mtoto wake mkubwa kwani mama yao alikuwa ametoka kwenda kazini kama kawaida.
Pingu
Image: Radio Jambo

Polisi huko Mwea wanamshikilia mwanamume mwenye umri wa miaka 42 kwa madai ya kumnajisi bintiye wa miaka miwili na nusu.

Chifu wa eneo hilo Henry Karuki alisema mshukiwa huyo inasemekana alinaswa Jumatatu na mtoto wake mkubwa kwani mama yao alikuwa ametoka kwenda kazini kama kawaida.

Kariuki alisema mtoto huyo alikimbizwa hospitalini ambako anahudumiwa.

"Mshukiwa alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi huku bintiye aliyekuwa akivuja damu alikimbizwa hospitalini ambako amelazwa," alisema.

Wakazi waliokuwa na hasira wamelaani kisa hicho huku wakitaka haki itendeke kwa mwathiriwa.

Charity Wambui, mkazi alisema alishtuka kwani hajawahi kusikia kisa kama hicho katika kijiji hicho.

 

Pia alitoa wito wa ulinzi wa watoto kutoka kwa wanyanyasaji wa ngono ambao wana nia ya kuharibu maisha yao ya baadaye

Naibu mkuu wa polisi katika eneo hilo Lucas Chebet aliiambia Sar kwa simu kwamba mshukiwa anazuiliwa na atafikishwa mahakamani baadaye.