logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hatuna uwezo kusitisha maandamano - Otiende Amollo

Otiende alisema timu ya Kenya Kwanza haijaondoa jina la Keynan kwenye orodha.

image
na Davis Ojiambo

Habari02 May 2023 - 11:27

Muhtasari


  • • Wiki iliyopita, Kenya Kwanza ilisema iko tayari kumwondoa mbunge wa Eldas Aden Keynan kwenye mazungumzo hayo.
Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo

Waakilishi wa muungano wa Azimio katika mazungumzo ya pande mbili wamesema hawana uwezo kusitisha maandamano yalioitishwa na viongozi wa muungano huo.

Wakihutubia wanahabari Jumanne, waakilishi hao wakiongozwa na Mbunge Otiende Amollo walieleza kuwa kamwe hawakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

"Kama kamati ya pamoja ya vyama viwili, hatukuwahi kupewa mamlaka ya kujadili chochote kuhusu maandamano. Sio katika nafasi yetu kuitisha au kusitisha maandamano," Otiende alisema.

Otiende alibainisha kuwa baadhi ya masuala yaliyoibuliwa na muungano wa Kenya Kwanza hayakuwa na msingi.

“Huwezi kumchukua mwanachama wetu ukamweka kwenye kamati kisha urudi na kutuambia tuondoe wetu ili na wewe ufanye hivyo hivyo haina mantiki,” alisema.

Wiki iliyopita, Kenya Kwanza ilisema iko tayari kumwondoa mbunge wa Eldas Aden Keynan kwenye mazungumzo hayo.

Katika kile kinachoonekana kama jaribio la kushawishi upinzani kusitisha maandamano yaliyopangwa, Kenya Kwanza ilisema Keynan ataondolewa ikiwa kutakuwa na mzozo wakati wa majadiliano.

Hata hivyo, Kenya Kwanza pia ilitaka wenzao wa Azimio pia kumwondoa Mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing kutoka kwa kamati hiyo.

Aidha, Otiende alisema timu ya Kenya Kwanza haijaondoa jina la Keynan kwenye orodha hiyo, na kuwataka Wakenya wasidanganywe.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved