logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkuu wa jeshi la Sudan anaonekana kwenye video ya kipekee akiwa na bunduki

Mapigano hayo yameingia mwezi wa pili ambapo zaidi ya watu 800 wameuawa.

image
na Davis Ojiambo

Habari18 May 2023 - 11:59

Muhtasari


  • • Mkuu wa jeshi na mpinzani wake kamanda wa RSF Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, maarufu kama Hemedti, wamejaribu kuongeza ari ya vikosi vyao vinavyopigana.

Jeshi la Sudan limechapisha video inayoonyesha kiongozi wake, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, akitembea kati ya wanajeshi waliokuwa wakishangilia katika eneo lisilojulikana katika mji mkuu, Khartoum.

Video hiyo ya nadra ya sekunde 23 iliyochapishwa siku ya Jumatano inaonyesha Jenerali Burhan akiwa na bunduki na bastola.Anaonekana akiwa amevalia mavazi ya kijeshi, akiwasalimia wanajeshi wanaomshangilia .

"Mpiganaji - Kamanda Mkuu wa Majeshi - kati ya askari wake uwanjani," kichwa cha habari cha video hiyo kilisema.

Hii ni video ya kwanza ya aina yake tangu mzozo unaoendelea wa kijeshi uanze tarehe 15 Aprili kati ya jeshi na na kikosi maalum cha (RSF).

Hata hivyo, katika siku za mwanzo za mapigano, Jenerali Burhan alionekana pamoja na viongozi wengine wa kijeshi wakiwaamuru askari kutoka ndani ya jengo lisilojulikana mjini Khartoum.

Mkuu wa jeshi na mpinzani wake kamanda wa RSF Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, maarufu kama Hemedti, wamejaribu kuongeza ari ya vikosi vyao vinavyopigana.

Hemedti pia alijitokeza katika eneo lisilojulikana huko Khartoum.Hivi majuzi pia alikanusha katika ujumbe wa sauti kwamba aliuawa.

Mapigano hayo ambayo yanachangiwa na mzozo wa madaraka kati ya Jenerali Burhan na Hemedti yameingia mwezi wa pili ambapo zaidi ya watu 800 wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved