Tisheni watu wengine lakini sio mimi-Uhuru kwa wakosoaji wake

Akizungumza siku ya Jumatatu, Uhuru alisema kuwa hatatikiswa na vitisho vyovyote.

Muhtasari
  • Uhuru aliendelea kuwaambia wajumbe kuwa mawazo yake yalimwambia angejiuzulu kutoka kwa chama kama kiongozi wa chama.
RAIS MSTAAFU UHURU KENYATTA WAKATI WA KONGAMANO LA KITAIFA LA JUBILEE 22/05/2023
Image: EZEKIEL AMING'A

Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta amemkashifu Rais William Ruto kuhusu jaribio la hivi majuzi la 'kuteka nyara' chama cha Jubilee.

Akizungumza siku ya Jumatatu, Uhuru alisema kuwa hatatikiswa na vitisho vyovyote.

"Kuna wale ambo wanadhani kazi ya ni ya vitisho . Lakini sasa wajaribu mwingine , sio mimi,"Alizungumza Uhuru wakati wa kongamano la kitaifa la chama cha Jubilee.

Uhuru aliendelea kuwaambia wajumbe kuwa mawazo yake yalimwambia angejiuzulu kutoka kwa chama kama kiongozi wa chama.

"Mawazo yangu yalikuwa yameniambia nipumzike kwenye siasa na kwenda kuhudhuria majukumu mengine. Nilidhani leo Nikiwa NDC ningejiuzulu na kusema kwamba muda wangu umekwisha nichague viongozi wengine," alisema.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa chama alisema kuwa Jubilee itasalia imara na kuungana kuwa kitu kimoja.

"Kustaafu sio kuchoka… ata wengine wanastaafu na nguvu zinaingozeka.Ata kama nimewacha siasa active, mimi bado ni mfuasi wa babaAkiniambia twende lazima twendwe."

Mnamo Februari mwaka huu, Uhuru alithibitisha msimamo wake katika Muungano wa Azimio La Umoja.

Alithibitisha kuwa yeye bado ni mwanachama wa Azimio La Umoja One Kenya Coalition Party, licha ya kimya chake.

"Ingawa nimestaafu siasa, bado ni mfuasi wa Raila. Akiniuliza twende lazima tufanye hivyo. Nilimuunga mkono na nitaendelea kufanya hivyo kwa sababu ninaamini ni mkweli," Uhuru alisema.

Mkuu huyo wa nchi Mstaafu amethibitisha kuunga mkono kinara wa Upinzani Raila Odinga na kusisitiza kuwa atamuunga mkono.

Huku akiwahutubia viongozi wapya walioteuliwa, aliwaonya dhidi ya kutoa matusi kwa wengine huku akiwaambia wanapaswa kuwa na heshima.

"Heshima sio utumwa, na ni mara mbili nipe heshima nikupe msiende kuwatusi wenjzenu tupeane heshima."