logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aliyekuwa Gavana wa Kiambu, Waititu adaiwa kuzimia nyumbani

Waititu anadaiwa kuanguka Jumapili akiwa nyumbani kwake na kukimbizwa hospitalini.

image
na

Habari05 June 2023 - 08:25

Muhtasari


•Wakili John Swaka alimweleza Hakimu Thomas Nzioki kwamba Waititu hangeweza kupatikana kortini kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi dhidi yake kwa sababu alilazwa hospitalini.

•Swaka alisema alipokea taarifa hiyo leo asubuhi lakini atatoa hati haraka iwezekanavyo.

Aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu

Mahakama ya Nairobi imefahamishwa kuwa aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu alianguka Jumapili akiwa nyumbani kwake na kukimbizwa hospitalini.

Wakili John Swaka alimweleza Hakimu Thomas Nzioki kwamba Waititu hangeweza kupatikana kortini kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi dhidi yake kwa sababu alilazwa hospitalini.

"Hatuko tayari kuendelea... Nilifahamishwa kwamba alianguka jana na kukimbizwa hadi Aga Khan ambako alilazwa," Swaka alisema.

Swaka zaidi alisema mke wa Waititu Susan Wangari hangeweza kufika kortini kwa sababu yuko naye hospitalini.

"Kwa hiyo, hatutaweza kuendelea na kesi leo," alisema.

Hakimu alisema hakuwa amepewa rekodi zozote za matibabu.

Swaka alisema alipokea taarifa hiyo leo asubuhi lakini atatoa hati haraka iwezekanavyo.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi kesho wakati Swaka anatarajiwa kuwasilisha stakabadhi za matibabu zinazoonyesha kuwa mteja wake yuko hospitalini.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved