logo

NOW ON AIR

Listen in Live

EPRA yaongeza bei za mafuta kwa Ksh13

"Kwa hiyo, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati ya Petroli (EPRA) imefanya mahesabu ya bei ya juu

image
na Radio Jambo

Habari30 June 2023 - 15:35

Muhtasari


  • Bei mpya za mafuta zitaanza kutumika kuanzia saa sita usiku Jumamosi, Julai 1, 2023, licha ya Sheria ya Fedha kusimamishwa.
Mhudumu akiweka gari Mafuta ya petroli

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) mnamo Ijumaa, 30, ilitangaza bei mpya za mafuta kwa Julai 2023.

Bei hizo zilipitiwa upya kufuatia kuongezeka maradufu kwa ushuru wa ongezeko la thamani (VAT) kwenye mafuta kutoka asilimia 8 hadi 16.

Jijini Nairobi, bei mpya zitauzwa kama ifuatavyo; petroli  Ksh195.53 kwa lita, dizeli Ksh179.67 na mafuta ya taa Ksh173.44 kwa lita.

Bei mpya za mafuta zitaanza kutumika kuanzia saa sita usiku Jumamosi, Julai 1, 2023, licha ya Sheria ya Fedha kusimamishwa.

"Kwa mujibu wa Sheria ya Fedha, 2023, Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye Super Petrol (PMS), Dizeli (AGO) na Mafuta ya Taa (IK) imefanyiwa marekebisho kutoka asilimia 8 hadi 16 kuanzia tarehe 1 Julai 2023.

"Kwa hiyo, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati ya Petroli (EPRA) imefanya mahesabu ya bei ya juu zaidi ya pampu ambayo itaanza kutumika kuanzia tarehe 1 Julai hadi 14 Julai 2023 kwa kuzingatia VAT kwa asilimia 16," ilisomeka sehemu ya taarifa ya EPRA.

“Madhumuni ya Kanuni za Upangaji Bei ya Petroli ni kupunguza bei za reja reja za mafuta ya petroli ambayo tayari yapo nchini ili uagizaji wa bidhaa na gharama nyinginezo zilizotumika kwa uangalifu zirejeshwe huku ikihakikisha bei nzuri kwa watumiaji.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved