Miguna ataka EACC kumchukua hatua kali na kutwaa mali ya gavana wa zamani wa Kakakamega Oparanya

Miguma alisema kuwa pia wanapaswa kutwaa tena kila kitu kitakachothibitika kuwa kimeibwa.

Muhtasari

Oparanya ni mshirika mkuu wa Kinara wa Upinzani Raila Odinga na amehudumu kwa miaka mingi kama naibu kiongozi wa Raila katika uongozi wa ODM.

 

akiwasili nchini kwa mara ya kwanza tangu alipofurushwa wakati wa serikali ya rais mustaafu Uhuru Kenyatta.
Wakili Miguna Miguna akiwasili nchini kwa mara ya kwanza tangu alipofurushwa wakati wa serikali ya rais mustaafu Uhuru Kenyatta.
Image: Andrew Kasuku

Wakili Miguna Miguna amepongeza Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) baada ya kumhoji aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kuhojiwa.

Oparanya na wakeze walihojiwa kuhusu madai ya ufujaji wa shilingi bilioni 1.3. Kulingana na Miguna, tume ya kupambana na ufisadi sasa inafaa kuwasilisha ushahidi madhubuti dhidi ya gavana huyo wa zamani.

Aliongeza kuwa pia wanapaswa kutwaa tena kila kitu kitakachothibitika kuwa kimeibwa.

"Mwanzo mzuri, EACC Kenya. Toa ushahidi thabiti. Chukuwa tena mali yote iliyoporwa na Oparanya wote," Miguna alisema.

EACC ilisema ilimwita gavana huyo wa zamani wa Kakamega kujibu maswali kuhusu Shilingi bilioni 1.3 zinazoshukiwa kufujwa enzi zake kama Gavana.

“Gavana huyo wa zamani aliitwa leo asubuhi katika Makao Makuu ya EACC ili kufafanua masuala kadhaa na kurekodi taarifa kuhusu uchunguzi unaoendelea,” taarifa hiyo ilisoma.

Tume hiyo pia ilibainisha kuwa uchunguzi wa kaunti hiyo ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea kuhusu madai ya kupotea kwa pesa za umma.

Oparanya alitumia muda mwingi katika makao makuu ya EACC akirekodi taarifa nao.

Mawakili wake awali walikuwa wamenyimwa idhini ya kuingia makao makuu ya EACC, pamoja na viongozi wengine kutoka muungano wa Azimio.

Maafisa wa upelelezi wa EACC walifanya uvamizi pacha katika nyumba mbili za Oparanya - katika mtaa wa Lang'ata Nairobi na katika nyumba yake ya mashambani katika kijiji cha Emabole, Butere.

Oparanya ni mshirika mkuu wa Kinara wa Upinzani Raila Odinga na amehudumu kwa miaka mingi kama naibu kiongozi wa Raila katika uongozi wa ODM.

Pia anahudumu kama mwenyekiti wa baraza kuu la muungano wa Azimio.