Arati ateuliwa naibu mwenyekiti wa kitaifa wa ODM huku chama kikitangaza mabadiliko ya NEC

Mwakilishi wa wanawake wa Kakamega Elsie Muhanda anachukua nafasi kutoka kwa aliyekuwa Mbunge wa Shinyalu Justus Kizito

Muhtasari
  • Seneta wa Migori Eddie Oketch atakuwa Katibu wa NEC wa Masuala ya Kibinadamu na Usimamizi wa Maafa.
Gavana wa kaunti ya Kisii
Gavana wa kaunti ya Kisii
Image: Facebook

Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kimefanya mabadiliko kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, chama cha Orange party kilitangaza kuwa Gavana wa Kisii Simba Arati sasa atahudumu kama Naibu Mwenyekiti wa Kitaifa, akichukua hatamu kutoka kwa aliyekuwa Mwakilishi wa Kike wa Kisii Janet Ong’era.

Mwakilishi wa Wanawake wa Busia Catherine Omanyo anachukua wadhifa huo kutoka kwa mtangulizi wake Florence Mutua kama Naibu Katibu Mkuu.

Mbunge wa Saboti Caleb Amisi ndiye Naibu Katibu Mwenezi mpya akichukua nafasi ya aliyekuwa mwakilishi wa mwanamke wa Kwale Zulekha Hassan.

Mwakilishi wa Wanawake wa Kwale Fatuma Masito ndiye Naibu Mweka Hazina mpya wa Kitaifa. Awali nafasi hiyo ilishikwa na aliyekuwa Mweka Hazina wa ODM Ogla Karani.

Seneta wa Migori Eddie Oketch atakuwa Katibu wa NEC wa Masuala ya Kibinadamu na Usimamizi wa Maafa. Anachukua nafasi ya mwanaharakati Bob Njagi.

Mwakilishi wa wanawake wa Kakamega Elsie Muhanda anachukua nafasi kutoka kwa aliyekuwa Mbunge wa Shinyalu Justus Kizito kama Katibu wa Usalama.