Mbunge wa Homa Bay Peter Kaluma kupinga uamuzi wa mahakama kuhusu LGBTQ

Kaluma anasema kwamba mahakama ya Kenya ndio kiungo dhaifu katika "vita dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

Muhtasari

• Kaluma alisema lazima mahakama ibadilishe uamuzi kuhusu LGBTQ. 

PETER KALUMA
Image: HISANI

Mbunge wa Homa Bay Town Peter Kaluma amesema atakwenda katika Mahakama ya Juu ya Kenya kupinga uamuzi kuhusu usajili wa miungano ya wapenzi wa jinsia moja LGBTQ na ufafanuzi wa tendo la mapenzi kama ilivyotumika katika kesi hiyo.

Mbunge huyo aliyezungumza waziwazi siku ya Jumatano alisema kuwa mahakama ya Kenya ndio kiungo dhaifu katika "vita dhidi ya mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya.

"Lazima tuirudishe kortini  na kuiomba mahakama kubatilisha uamuzi wake," Kaluma alisema.

 Mahakama ihakikishe kuwa asili ya tendo la mapenzi ni baina ya mume na mke hali inayobainika wakati wa kuzaliwa.

 Mbunge huyo alisema kuwa Kenya lazima ipitishe Mswada wa kulinda Familia haraka iwezekanavyo ili kukomesha "kichaa cha LGBTQ.

"Mafanikio yetu mbele ya mahakama hayatakuwa rahisi, lakini ni jambo sahihi, kuokoa ubinadamu," aliongeza.

Lazima tuharakishe kupitishwa kwa mswada wa ulinzi wa familia, ili kumaliza wazimu huu.

Mbunge huyo pia alisema kuna mswada bungeni unaolenga kuharamisha uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, kamati husika ilipaswa kuzingatia Muswada huo ndani ya siku thelathini, lakini miezi kadhaa baadaye, bado haujashughulikiwa.

Kaluma akiri kuwa vita dhidi ya LGBTQ sio rahisi lakini hatalegeza juhudi zake ataendelea kushinikiza ili kuharamisha mapenzi ya jinsia moja.

 

Mbunge huyo alidai kupokea vitisho kwamba hataruhusiwa kusafiri katika mataifa ambayo mahusiano ya watu wa jinsia moja ni halali.

“Nimetishwa hata kuwa sitapewa visa kusafiri hadi nchi ambazo zimeruhusu jambo hili potovu,” aliongeza...hata nilipokwenda mahakamani nilikwenda nikijua tutashindwa, hata tukirudi tunaenda kuwatia aibu tu, lakini vita hii tutashinda,” alisema.