Aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga anadaiwa kutekwa nyara

Kulingana na wake, Wakili Ndegwa Njiru alitekwa nyara kutoka kwa nyumba yake huko Kiambu Jumamosi usiku.

Muhtasari
  • Mnamo Mei, iliripotiwa kuwa polisi walivamia nyumba tatu za Maina Njenga katika kaunti za Nairobi, Nakuru, na Laikipia.
  • Alishtakiwa kwa kupatikana na rungu za Kimasai, pinde na mishale miongoni mwa mambo mengine.
Maina Njenga
Maina Njenga
Image: STAR

Aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga amedaiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana ndani ya mji wa Kiambu.

Kulingana na wake, Wakili Ndegwa Njiru alitekwa nyara kutoka kwa nyumba yake huko Kiambu Jumamosi usiku.

"Mteja wangu Maina Njenga ametekwa nyara na DCI kutoka kwa nyumba yake huko Kiambu....Amepelekwa eneo lisilojulikana," alichapisha kwenye ukurasa wake wa X.

Gazeti la Standard liliripoti kuwa kakake Njenga, Njoroge Kamunya, alisema kiongozi huyo wa zamani wa Mungiki alitolewa nje ya gari lake.

Mnamo Mei, iliripotiwa kuwa polisi walivamia nyumba tatu za Maina Njenga katika kaunti za Nairobi, Nakuru, na Laikipia.

Mnamo Julai, kiongozi huyo wa zamani wa Mungiki alidaiwa kukamatwa na polisi aliokuwa eneo la chini la Matasia, Ngong na kupelekwa eneo lisilojulikana.

Maina Njenga baadaye alifikishwa katika mahakama ya Makadara baada ya kuwa kizuizini.

Alishtakiwa kwa kupatikana na rungu za Kimasai, pinde na mishale miongoni mwa mambo mengine.

Hati ya mashtaka ilisomeka kuwa mnamo Julai 20, 2023, huko Kiserian ndani ya Kajiado, bila visingizio vya msingi, watatu hao walipatikana na silaha za kushambulia; mapanga 14, panga 24 za kimasai, rungu 46 na fimbo tatu za jembe.

Hati ya mashtaka ilisema hali hiyo iliibua dhana nzuri kwamba silaha hizo za kukera zilikusudiwa kutumiwa kwa njia inayoathiri utulivu wa umma.