Shule yatozwa Sh4.5m kwa kutumia picha za watoto bila idhini

Shule ya Roma yenye makao yake mjini Uthiru, Nairobi, inadaiwa kuchapisha picha za watoto wadogo bila idhini ya wazazi.

Muhtasari

• Kulingana na kamishna wa Data hii ni adhabu ya kwanza na ya juu zaidi kwa kituo cha elimu kutolewa.

• Walibainisha taasisi  zitapata somo kutokana na adhabu ya kutotumia takwimu za watoto wadogo bila idhini ya wazazi.

wanafunzi wa Roma school Uthiru picha Roma school Uthiru /facebook
wanafunzi wa Roma school Uthiru picha Roma school Uthiru /facebook

Ofisi ya Kamishna wa Kulinda Data imeipiga faini taasisi ya elimu kwa kukosa kutii Sheria ya Kulinda Data.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, Shule ya Roma yenye makao yake mjini Uthiru, Nairobi, inadaiwa kuchapisha picha za watoto wadogo bila idhini ya wazazi.

  Kulingana na kamishna huyo, hii ni adhabu ya kwanza na ya juu zaidi kwa kituo cha elimu kutolewa.

Walibainisha taasisi hizo zitapata somo kutokana na adhabu ya kutotumia takwimu za watoto wadogo bila ridhaa ya wazazi.

"Hii inatuma ujumbe kwa shule na vituo vingine vinavyoshughulikia data za watoto ili kupata ridhaa kutoka kwa wazazi/walezi kabla ya kuchakata data za watoto," inasomeka taarifa hiyo.

Mkurugenzi wa shule hiyo, alisema hajapokea malalamiko yoyote kuhusu kutolewa kwa picha za watoto hao. "Nilipokea barua kutoka kwa ofisi ya ulinzi wa data lakini sielewi kinachoendelea kwa sababu sijapokea malalamiko yoyote kutoka kwa mtu yeyote kuhusu suala hilo," alisema.

Aliongeza kuwa atatembelea afisi ya kamishna wa ulinzi wa data kufuatilia suala hilo. “Itanibidi niende katika ofisi zao,” alisema.

Kulingana na ofisi ya kamishna wa data, notisi za adhabu zimetolewa kwa mujibu wa Kifungu cha 62 na 63 cha Sheria ya Ulinzi wa Data, 2019 (Sheria) na Kanuni ya 20 na 21 ya Kanuni za Ulinzi wa Data (Taratibu za Kushughulikia Malalamiko na Utekelezaji), 2021.

Kamishna wa Data Immaculate Kassait alihimiza mashirika kufuata Sheria ya Ulinzi wa Data kwa kutekeleza kanuni na ulinzi wa data.

Pia alitoa wito kwa wadhibiti wa data na Wachakataji Data kuhakikisha kuwa usindikaji wa data za kibinafsi unaendana na kifungu cha Sheria. "Kushindwa kuzingatia Sheria kutasababisha kuanzishwa kwa taratibu za utekelezaji," Kassait alisema.