Wafanyakazi 2 wa Kenya Power wakamatwa kwa kudai hongo ya Ksh.50k ili kurejesha umeme

Wanapaswa kushtakiwa kwa makosa ya hongo.

Muhtasari
  • Lawrence Njogu na Patrick Onsare walinaswa Jumatano na maafisa wa upelelezi kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) baada ya mlalamishi kuripoti suala hilo kwa shirika la kupambana na ufisadi.
Pingu
Image: polisi wawili washikwa kwa madai ya hongo

Wafanyakazi wawili wa Kenya Power wamekamatwa kwa kuitisha hongo ya Ksh.50,000 ili kurejesha usambazaji wa umeme, ambao walikuwa wamekatiza hapo awali, katika nyumba moja huko Kawangware.

Lawrence Njogu na Patrick Onsare walinaswa Jumatano na maafisa wa upelelezi kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) baada ya mlalamishi kuripoti suala hilo kwa shirika la kupambana na ufisadi.

Walinaswa mara baada ya kupokea kiasi hicho kutoka kwa mlalamishi.

"EACC ilithibitisha madai hayo na kufanya oparesheni iliyopelekea kukamatwa kwa washukiwa huku wakipokea kiasi kilichohitajika," kilisema chombo hicho cha kupambana na ufisadi.

Washukiwa hao walizuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani na leo (Alhamisi) walirejeshwa katika Kituo cha Polisi cha EACC Integrity Centre ambako wanashughulikiwa kwa sasa.

Wanapaswa kushtakiwa kwa makosa ya hongo.