Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA) imetoa wito kwa Wakenya kuchukua fursa ya muda wa kazi ulioongezwa ili kuchukua namba pleti na leseni za udereva.
Meneja wa usalama wa Barabarani wa NTSA Samuel Musumba amesema hatua ya kuongeza muda wa saa za kazi ilitokana na mahitaji makubwa ya namba pleti za kisasa.
NTSA siku ya Ijumaa iliongeza saa zake za kazi katika juhudi za kukidhi mahitaji ya wananchi wanaotuma maombi kupata namba pleti za kisasa na wale wanaotaka leseni ya kuendesha magari.
Katika agizo hilo lililotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, ofisi zao sasa zitafanya kazi kwa takribani saa 11, kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
Ofisi hizo pia zitaendelea kuwa wazi kwa saa nane, kwa Jumamosi mbili zijazo.
Msumba alisema mahitaji makubwa ya namba pleti na leseni za udereva yameifanya mamlaka hiyo kuhudumia maelfu ya watu kutokana na ongezeko la mahitaji.
"Mahitaji ya namba pleti na leseni za kuendesha gari yamekuwa makubwa kwa hivyo tulisema kusaidia Wakenya na kufanya huduma karibu na watu, tunahitaji kuongeza saa za kazi kidogo," Msumba alisema.
"Tunaomba Wakenya wengi iwezekanavyo tafadhali kuchukua fursa ya saa zetu za ziada, njoo tukuhudumie, tuna madawati ya huduma sasa kila mahali, maswala yoyote sasa tutayashughulikia huna haja ya kuwa na wasiwasi," Musumba alisema.
Chini ya saa mpya za kazi, Majumba na Ofisi zote za za NTSA zitafanya kazi Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa moja unusu asubuhi hadi saan kumi na mbili jioni.
Zaidi ya hayo, ofisi zitaendelea kuwa wazi kwa umma siku ya Jumamosi, Septemba 30, 2023, na Jumamosi, Oktoba 7 2023 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni ili kuondoa mrundiko.