logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto apongeza UN kwa kuruhusu Kenya kuongeza juhudi za kudumisha amani Haiti

Bahamas imejitolea maafisa 150 huku Jamaica, Antigua na Barbuda zikiahidi kusaidia.

image
na Radio Jambo

Makala03 October 2023 - 13:43

Muhtasari


• Kenya imejitolea kutuma wanajeshi 1,000 nchini Haiti, huku Bahamas ikiwa imejitolea maafisa 150 huku Jamaica, Antigua na Barbuda zikiahidi kusaidia.

Rais William Ruto amepongeza idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukubali vikosi vya kigeni kuhudumu nchini Haiti ili kudhibiti ghasia za magenge ya kihalifu ambayo yametikisa mji mkuu wa nchi hiyo Port-au-Prince kwa zaidi ya mwaka mmoja. 

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumanne, Rais Ruto alikaribisha uamuzi wa baraza hilo, akiutaja kuwa " chombo muhimu cha kufafanua juhudi za kimataifa kudumisha usalama nchini Haiti. 

"Hali ya Haiti inadai, kama suala la kuzingatia kibinadamu, uwajibikaji wa kimaadili na haki ya kimsingi, kwamba hatua zinapaswa kuongezwa kwa kiasi kikubwa ili kukidhi mahitaji ya misaada ya dharura, misaada ya kibinadamu, afya ya umma na ulinzi,” Rais Ruto alisema. 

Baraza hilo lenye wanachama 15 mnamo Jumatatu lilipitisha azimio linaloidhinisha 'oparesheni ya Usalama wa Kimataifa chini ya uongozi wa Kenya kusaidia polisi wa Haiti katika kupambana na magenge hayo. Azimio hilo lililoandaliwa na Marekani na Ecuador, liliidhinishwa kwa kura 13  huku China na Urusi zikijizuia kupiga kura. 

Aliitaja hatua ya Kenya kuwa ni uthibitisho wa kujitolea kwa Afrika pamoja na sera ya Umoja wa Afrika ya mshikamano wa Wafrika inayofungamana na historia ya ukoloni wa Afrika. 

“Kwetu sisi nchini Kenya, jukumu hili ni muhimu na dharura. Tulipitia mateso makali ya ukoloni, pamoja na mapambano ya muda mrefu , magumu na ya kukata tamaa ya kupigania uhuru dhidi ya wakoloni,” alisema Ruto. 

Kenya imejitolea kutuma wanajeshi 1,000 nchini Haiti, huku Bahamas ikiwa imejitolea watu 150 huku Jamaica, Antigua na Barbuda zikiahidi kusaidia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved