Rais William Ruto amemteua aliyekuwa Seneta Isaac Mwaura kuwa msemaji wa serikali.
Mwaura atasaidiwa na Bi Mwanaisha Chidzuga na Gabriel Muthuma
Uteuzi huo ambao utaanza kutumika mara moja ulitangazwa Jumatano jioni na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei.
Kabla ya kuteuliwa kuwa msemaji wa Serikali, Mwaura alikuwa ameteuliwa na Rais Ruto kuwa Katibu Mkuu wa Utawala (CAS) katika Ofisi ya Waziri Mkuu Musalia Mudavadi.
Alikuwa bado kushika wadhifa wa CAS kufuatia uamuzi wa mahakama uliosimamisha uteuzi wa CAS.