Mwanamuziki Naira Marley azuiliwa kwa kifo cha MohBad

MohBad alikufa kwa njia isiyoeleweka katika hospitali ya Lago na akazikwa haraka na familia yake.

Muhtasari

•Msemaji wa polisi wa Lagos Benjamin Hundeyin alisema kuwa Marley anazuiliwa "kwa mahojiano na shughuli zingine za uchunguzi".

Image: BBC

Polisi wa Nigeria wamemshikilia mwimbaji na mtunzi wa nyimbo Naira Marley kuhusiana na kifo cha nyota wa Afrobeats MohBad.

Msemaji wa polisi wa Lagos Benjamin Hundeyin alisema kuwa Marley anazuiliwa "kwa mahojiano na shughuli zingine za uchunguzi".

Marley alishiriki kwenye mtandao wa X kwamba alikuwa akisaidia mamlaka katika uchunguzi wa kifo cha MohBad na alikuwa "akikutana na polisi akiwa na matumaini ya ukweli kufichuliwa na haki kutendeka".

MohBad alikufa kwa njia isiyoeleweka katika hospitali ya Lagos mnamo Septemba 12 na akazikwa haraka na familia yake.

Kifo cha nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 kilizua maandamano na kutaka uchunguzi kutoka kwa mashabiki wake, jambo ambalo lilipelekea polisi kuufukua mwili wake kwa uchunguzi.

Mashabiki walielekeza hasira zao kwa Marley, ambaye alikuwa amesaini MohBad chini ya lebo yake ya muziki ya Marlian Records.

MohBad aliondoka kwenye lebo hiyo mwaka jana, baada ya kutofautiana na Marley.

Kufuatia kifo chake, video kadhaa za MohBad akilalamika kuhusu uhusiano wake na Marlian Records ziliibuka tena.