Esma afunguka kuhusu madai ya ugomvi na kakake Diamond

Muhtasari

• "Kwa kweli kuna mengi yanasemwa kwenye mitandao, wengi wa wafuasi wetu kwenye mitandao ya kijamii wanachochea chuki kati yangu na Diamond

Esma Platnumz na Diamond

Baada  ya kuwa na tetesi nyingi kwenye  mitandaoni  ya kijamii  kwa muda mrefu kwake Diamond Platnumzs kutokuwa na maelewano na Dadake Esma, dadake amejitokeza kuzungumzia suala hilo.

Esma Platnumzs mfanyibiashara nchini Tanzania ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo amefichua kuwa na uhusiano mwema na kakake mdogo ambaye ni msanii maarufu wa muziki wa Bongo Diamond Platnumz.

Kupitia kituo cha Wasafi FM kuna uvumi kinachomilikiwa Diamond walizugumza moja kwa moja na Esma Platnumz's ili kuweka wazi mambo.

"Kwa kweli kuna mengi yanasemwa kwenye mitandao, wengi wa wafuasi wetu kwenye mitandao ya kijamii wanachochea chuki kati yangu na Diamond ila yote ni uongo mimi na kakangu tuko salama na uhusiano wetu ni mema kwa hivo watu kwenye mitandao wawache kuingilia  familia ." alisema Esma.

Baada ya mwana habari kutaka kujua zaidi iwapo Diamond humtembela nyumbani kwake, Esma alisimulia kwamba wanapendana kama ndugu na dada akikiri siku ya kusherekea kuzaliwa kwa kakake Diamond walisherekea nyumbani kwake wakiwa na mama yao Mama Dangote.

"Diamond ni mtu mkarimu sana mara mingi napata zawadi kutoka kwake pia mara kwa mara tunatembeleana katika vikao vya familia ". alisema.